Mpango

Tunafunza familia kiutendaji, kijamii, desturi ya afya ya umma katika lishe, ukulima endelevu, kiasi, maji na usafi  kwa lengo la kuwa na chakula cha kutosha, kuboresha afya na ustawi wa familia.

Hamasa yetu

Ni nini kinachotupatia motisha? Yesu alisema ya kwamba alikuja ili tuwe na uzima na tuwe nao tele. Tunaamini kwamba anatamani chanzo cha maisha kianzie hapa na sasa na alikusudia wafuasi wake waweze kushiriki uzima na watu wote

Utume kwa ulimwengu

Lengo letu kuu ni kushiriki katika upendo wa Yesu na watu wote. Tunafanya hivyo kwa kuzingatia "viungo" vyetu vinane vya afya na ustawi. Kila tunachofanya kimethibitishwa na kiko kwenye misingi ya Biblia.

Viungo

Kusaidia watu kujisaidia wenyewe na wengine kwa kichocheo cha maisha tele

Kwa kuchunguza sababu zinazochangia kusababisha maeneo ya kimataifa ya afya na maisha marefu, tumeendeleza FARM STEW, kichocheo rahisi, lakini chenye nguvu kwa maisha mengi. Vipawa vyako husaidia watu kujisaidia kupitia "viungo" rahisi, vinavyotoa maisha tele. Wafadhili wanaoshirikiana na FARM STEW huwaandaa wakufunzi kwenda nje na kutoa mafunzo kwa familia maskini na watu walio katika mazingira magumu ili waweze kustawi kwa mikono yao wenyewe! Dhamira ya FARM STEM ni kuziwezesha familia kupambana, kuzuia njaa, magonjwa na umaskini. Viungo hivyo nane ni:

Ukweli wa kushangaza Mahojiano ya STEW na Mchungaji Doug Batchelor

Mpango wetu wa majaribio

Ilianzishwa mwaka wa 2015

FARM STEW Uganda

Uganda ina miliki mchanganyiko wa kipekee wa maliasili ambazo hutoa uwezo mkubwa. Maji safi ni tele, takriban asilimia thelathini na nne (34%) ya  ardhi  ni  yenye rutuba, na hali yake ya hewa  inaruhusu misimu miwili au hata mitatu ya mavuno kwa mwaka.  Ijapokuwa 
-Alisimia sitini na moja (61%) ya Waganda huishi chini ya dola ($ 2%) kwa siku
-Asilimia thelathini na tano (35%) ya watoto wa Kiganda wana lishe duni, na
-Watoto wanaoishi mashambani wana kiwango cha juu  cha kifo kinachozidi asilimia arubaini na tano (45%) 

FARM STEW inaona uwezo katika nchi ya Uganda. Mafunzo yetu huwaandaa watu wasio na uwezo kwa kuwapa ujuzi muhimu ili kuboresha maisha yao na nchi yao kwa ujumla.

Kufikia sasa, timu yetu yenye washikiri 7 Waganda imewapa mafunzo zaidi ya watu18,000. Tunawafikia familia moja, kijiji kimoja kwa wakati.

KILIMO
MTAZAMO
PUMZIKO
MILO
USAFI
KIASI
UJASIRIAMALI
MAJI