Usafi

Kukuza usafi
Mamilioni hukumbwa na kifo kila mwaka kutokana na ukosefu wa msingi wa usafi na usafi wa mazingira.
Wasichana wanalazimishwa kutoka shule na kuaibika kwa hali ya ukomavu wa miili yao.
Maelezo ya msingi ya maambukizi ya magonjwa na vifaa vya usafi vinaweza kuwasaidia wote.
Wanawake na wasichana wengi ulimwenguni hawana uwezo wa kupata visodo,vyoo safi vya binafsi au njia safi za kujitunza wakati wa hedhi. Wengi huwa na aibu kubwa na wengine hata kuacha shule ambapo huchangia katika tofauti za elimu ya kijinsia. Zawadi zenu hutoa uhuru kutokana na aibu. (Bonyeza ili kujifunza)
Uelewaji kimsingi wa maambukizi ya ugonjwa husaidia wanakijiji kuwa na ufahamu kwamba usafi ni muhimu kwa afya. Elimu ya usafi inahamasisha watu wa jamii kurekebisha tabia zao, kama vile kuosha mikono kwa njia ifaayo na mbinu za kuosha vyombo.
Tunatumia mbinu shirikishi ya kijamii ambayo inawatia motisha wenye nyumba ili kujenga, kudumisha na mara kwa mara kutumia vyoo vyao wenyewe, mrundiko wa taka na mbolea. Jambo hili hutenga vitu visivyokuwa safi kutokana na vilivyo safi, kanuni ambayo ni muhimu katika kuokoa maisha.
Miradi yetu ya usafi
Hapo chini kuna baadhi ya miradi tunayoendeleza kwa sasa na njia unazoweza kuhusika.