Chakula

Kula kiafya
Kazi ya kupanga, kukuza, kuandaa na kusafisha baada ya chakula ni kazi ya upendo na kazi ya msingi ya wanawake wengi duniani kote. Tendo la kula pamoja na wengine hukuza afya kimwili na kisaikolojia.
FARM STEW inakuza uzalishaji wa vyakula vyenye virutubishi vya kutosha ili kuangazia upungufu mwilini uletwao na vyakula kama vile machungwa, viazi tamu vilivyo na virutubishi vingi vya vitamini ya "A" na mahuluti ya maharagwe yanayoongeza madini ya chuma.
Maharagwe ni ya ajabu! Sio tu kwa kuupa mwili madini ya protini ya juu, mafuta na madini ya chuma bali huupa udongo rutuba pia.
Kipimo kimoja cha chakula cha mikunde (jamiiya maharagwe) kwa siku huongeza miaka 4 zaidi ya maisha.
Maharagwe ya soya huwa na protini ya ubora wa hali ya juu na yanayopatikana na kutumiwa kwa njia tofauti. Tunafundisha njia mbadala za kutumia maharagwe haya yenye nguvu na kuifanya soya kuwa ya maana kama chungu chenye lishe ya dhahabu.
Kwa kula upinde wa mvua wa matunda na mboga katika wigo wa rangi ya asili, unaweza kuhakikisha mahitaji yako madogo ya lishe yanafikiwa na chakula unachokula.
"Upinde wa mvua" bandia wa rangi bandia na ufungaji mara nyingi ni vyakula ambavyo vina thamani ndogo kwa afya ya binadamu.
Njia ya Mungu dhidi ya njia ya mwanadamu? Ni nani lengo lako katika maisha tele?
Tunahimiza vyakula vya kitropiki vilivyopo ambavyo vinaweza kupandwa kwa urahisi na familia zinazohitaji zaidi.
Tunafundisha madarasa ya upishi kiutendaji yanayolenga utengenezaji wa vyakula nyumbani na mbinu za uhifadhi ili kuimarisha upatikanaji wa virurubishi vya madini kwa mwaka kwa miaka yote.
Kila mtu anashiriki na kila mtu anafurahia!
Miradi yetu ya chakula
Hapo chini kuna baadhi ya miradi tunayoendeleza kwa sasa na njia unazoweza kuhusika.