Kilimo

Kudumisha Mashamba na Jamii
Tunafundisha mbinu za ukulima ambazo zinalenga kilimo hai, kilimo endelevu na ambazo zimeendelezwa Afrika kupitia Misingi ya Ukulima Tunazisaidia jamii kuanzisha mashamba madogo ya mboga za jikoni, kuwaonyesha kutengeneza mbolea, kuhimiza na kuwa na jitihada katika kilimo ambacho kinaweza kuleta faida.
Kila kitu tunachokifanya lazima kifanywe kwa wakati, kwa kiwango cha juu, bila uharibifu na kwa furaha. Kwa kanuni hizi, wakulima wadogo wanaweza kufurahia fadhila ya dunia.
Tunaamini kuwa wakulima wa mashambani katika vijiji kote ulimwenguni wanaweza kuwa na maisha tele kwa kujifunza kutunza ardhi vizuri kwa njia inayostahili. Tunafanya kazi kuwafundisha mbinu bora zaidi za ukulima.
Asilimia 98 ya wenye njaa duniani wanaishi katika nchi zinazoendelea.
Asilimia 75 kati yao wanaishi vijijini, hasa katika vijiji vya Asia na Afrika, na
Asilimia 70 kati yao wanategemea kilimo kama kazi yao.
Ndiyo sababu tumejitolea kuwafikia, kuandaa na kuwatia moyo.
Angalau watoto milioni mia moja hamsini na sita (156,000,000) ulimwenguni kote wamedumaa na athari za maisha mabaya ya afya na matatizo ya mapato. Walio chini ya lishe bora huchangia zaidi ya thuluthi moja ya vifo vyote. Kwa kuwafundisha ukulima wa kifamilia tunatafuta kupambana na udumavu wa watoto katika ulimwengu wote.
Mipango yetu ya ukulima
Hapo chini kuna baadhi ya miradi tunayoendeleza kwa sasa na njia unazoweza kuhusika.