Yako 
 Mwongozo wa  ustawi
F

Kulima kunakupata nje ukifanya mazoezi katika hewa safi na mwangaza wa jua mpango wenye uponyaji na uzima. Jua liwakalo litaua virusi katika muda wa dakika 30 tu. Uhai umo katika damu na hewa safi hututakasa kusafisha mapafu. Udongo una maelfu ya spishi ya vidudu ambavyo baadhi  huchochea kazi ya kinga, hasa katika mapafu. Kama unataka usaidizi kujifunza kuhusu ukulima , www.borntogrow.net ina mafundisho mengi.

A

Mfumo wa kinga hukua kwenye mifupa. Hofu,tisho  na huzuni (Zaburi 6:2) huharibu, lakini  moyo wenye furaha hufufua roho iliyopondwa na kuimarisha mifupa. (Mithali 17:22) Msamaha, shukrani na uaminifu katika Mungu huleta amani na kuimarisha mfumo wa kinga. Kuimba kwa Bwana wimbo wa shukrani hata wakati mgumu huhakikishia na kutuliza nafsi amani na tumaini katika ulimwengu huu wa dhambi. Zaburi 100: 4-5, 118:1, 69:30

R

Hakuna kitu kinachoboresha kazi ya mfumo wa kinga kama masaa 8 ya kulala. Wakati wa kulala, mwili hufanya kaitokiniaina ya protini na seli za kinga ambazo hulenga maambukizi na uvimbe. Ukosefu wa usingizi usiku au asubuhi na mapema na ukosefu sugu  wa usingizi hupunguza kazi ya kinga kwa kiasi kama nusu. Usingizi mdogo husaidia pia.Yesu asema,"Njooni kwangu . . . na nitawapumzisha"  (Mathayo 11:28)

M

Chakula cha mimea kisichokobolewa ndio ufunguo wa kinga imara. Resheni tisa za rangi ya kina ya vyakula vyenye virutubishi vingi hutoa vizuia oksidi na virutubishi vidogo vinavyohitajika kwa ajili ya mfumo imara wa kinga. Itatoa takriban 1500 miligramu za vitamini C  kwa siku,kinga imara ya mwili. Vitamini D3 (4,000 IU) na zinki ( miligramu 25) kila siku pia husaidia. Epuka sukari. Inaharibu  seli za kinga kwa saa kadhaa baada ya kuila. Mafuta ya mgando na  mafuta ya maji  hupunguza oksijeni na kuzinyima chakula seli zinazopigana mwilini.

S

Lengo kuu katika kuepuka magonjwa ya kuambukiza ni kupunguza idadi ya viini hai vinavyokushambulia. Hii  hutimilika vizuri hasa; 1) kwa nia ya kuosha mikono kwa sabuni, kusugua na maji mengi 2) wakati wa mgogoro huu wa sasa kuvaa barakoa, hata kama ni kitambaa cha  bandana ili kuziba  pua na kinywa, hutumika kama kizuizi kupunguza virusi na bakteria na kupunguza  kugusa uso wako. Hatua hizi ' Mpende jirani yako kama nafsi yako. ' (Mt. 22:39).

T

Kula na kunywa kwa busara ni muhimu sana hasa wakati unahitaji kulinda mfumo wako wa kinga. Uvutaji sigara na uvutaji mvuke wake huharibu  seli katika mapafu yako zinazohitajika kwa ajili ya mapumuo bora. Pombe na dawa zingine ya burudani  huwa na  uwezo wa kuathiri kufanya maamuzi ya busara  wakati huu muhimu. Ili kupambana na  ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza, tunahitaji kuboresha ubongo wetu pamoja na miili yetu. Mtukuzeni Mungu katika miili yenu (1 Wakorintho 6:19, 20)

E

Nia ya kufanya kazi yenye changamoto kwa uvumilivu na bidii ni ufunguo wa biashara. Lengo la biashara halipaswi kuwa na utajiri, bali kuwa tajiri katika matendo mema (1 Timotheo 6: 17-19). Kulisha na kutunza familia yako mwenyewe hutoa heshima ambayo haina thamani. Kuzindua biashara ambayo inaweza kuajiri na kukimu watu wengine inaweza kuwa baraka kwa wengi.

W

Maji kama barafu, kioevu, na mvuke ni vitu visivyoweza kubadilishwa katika  kupambana na ugonjwa wa kuambukiza hasa ya mfumo wa kupumua. Kunywa lita 2 hadi 3 za  maji kila siku na zaidi kama u mgonjwa au una joto jingi. Kwa hiari tumia maji  kuchochea mzunguko na kuamsha seli za kinga. Hii inaweza kufanyika kwa kuoga maji moto na baridi (kubadilisha mara 3 kwa dakika 3 moto,  sekunde30 baridi). Kuosha miguu kwa maji moto na baridi  huleta msuguano wa kuvuta mvuke.

Kwa maelezo zaidi kuhusu masomo haya tafadhali nenda kwa: www.farmstew.org/post/10-Free-Things-You-can-do