Kujitolea
Kujitolea kwetu
Ni kwa wale Wanaotuhitaji Sana
Tumejitoa kikamilifu kwa afya ya kijumla ya familia za mashambani zenye kilimo cha kujikimu na kijiji. Mbinu zetu ni rahisi, za kivitendo. Tunaondoa vizuizi vya lugha na Kisomo kwa kufanya kazi kupitia kwa timu za wenyeji kwa kutumia picha za watu ili kuwasiliana wakati wa mafunzo na kuwaandaa viongozi wa jamii kuweza kuwafunza wengine.
Kujitolea kwetu kwa maskini kunaakisi ya Kristo ambaye alikuja kuleta habari njema kwa maskini. Kwa kuwahudumia wale walio na njaa, yatima, wakimbizi na wafungwa, tunamtumikia Kristo Mwenyewe.
Kwa maskini
Kwa sayari
Kwa kuhimiza kilimo endelevu na vyakula vitokanavyo na mimea, FARM STEW inatenda kwa niaba ya sayari yetu. Tunaamini kwamba tumeitwa kuwa wasimamizi wa uumbaji, tukijua kwamba misimu yake ya nyakati za majani na mavuno ni muhimu kwa maisha ya binadamu.
Kwa Mungu
Hatimaye, tunawatumikia wengine kwa sababu tunajua kwamba wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Kila uhai, kutoka wakati wa kushika mimba hadi kifo, unastahili juhudi za kuendelezwa, kuboreshwa na kuimarishwa, kimwili na kiroho. Kwa kuwaheshimu wengine, tunamheshimu Mungu ambaye alionyesha upendo wake kwetu kwa uwazi zaidi kupitia kwa Yesu.