Ilichapishwa
Desemba 23, 2020

Marudio ya mwisho wa Mwaka - Mwaka wa NDIYO!

Joy Kauffman, MPH

Furahia safari ya video ya dakika ya 6 duniani kote kwa kubonyeza hapo juu.

Hapa ni toleo la Kihispania!! (Huellas de FARM STEW en el 2020)

Asante kwa kubadilisha maisha ya Christine na FARM STEW, Klabu ya Akiba katika Kambi ya Wakimbizi ya Pagirinya kwa zawadi zako za ukarimu!

Christine ni mmoja wa wajane wengi katika kambi ya wakimbizi ya Pagirinya waliopoteza waume zao katika vita vya Sudan Kusini mwaka 2016. Baada ya kifo cha mumewe alijitahidi kujikimu na watoto wake wanne akitegemea tu msaada mkubwa uliotolewa na Umoja wa Mataifa. Wakati FARM STEW ilipofika kwenye kambi yake ya wakimbizi mwezi Novemba 2018, walisaidia kuanzisha klabu ya akiba. Christine aliamua kujiunga.

Mwaka mmoja baadaye, wakati klabu ya akiba ilipokutana kusambaza fedha zao, alipokea zaidi ya shilingi 300,000 za Uganda (zaidi ya dola 80 za Marekani). Mara moja alichukua fedha hizi na kuwekeza katika biashara ndogo ndogo katika kituo cha biashara cha Pagirinya ambapo sasa ana uwezo wa kupata pesa za kutosha kusaidia familia yake. "Sasa ninaweza kumudu mahitaji ya msingi ya watoto wangu," alisema Christine. Hivi karibuni, akizungumza na mkufunzi wa FARM STEW Amon, Christine alisema kuwa bado anashiriki katika klabu ya akiba na anatarajia usambazaji ujao wa fedha.

"Mipango mikubwa inangojea!" alisema. 

Klabu ya Akiba  katika Kambi ya Wakimbizi ya Pagirinya

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Joy Kauffman, MPH
Joy ni mwanzilishi mwenye shauku wa FARM STEW.
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.