Ilichapishwa
Juni 20, 2019

Siku ya wakimbizi duniani 2019: 'Kipindi Chako, Sauti Yako '

Joy Kauffman, MPH

 Ni siku ya wakimbizi duniani 2019: 'Hedhi yako, Sauti yako '
Jitihada mpya za uzinduzi katika makazi ya wakimbizi unaotoa fursa kwa wanawake na wasichana  kusimamia hedhi zao kwa heshima.

Mnamo tarehe 20 Juni, mpango mpya; 'Hedhi yako, Sauti yako' itazinduliwa na kusambaza 900 AFRIpads kifurushi kikubwa cha vifaa vya hedhi katika makazi ya wakimbizi kaskazini mwa Uganda. Uzinduzi wa kampeni ni kufuatia maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani na ni ushirikiano wa pamoja kati ya AFRIpads, Lunapads na FARM STEW. Mchango wa awali wa vifaa 200 utafanyika leo pamoja na lengo la awali juu ya wasichana  waliohitimu  umri wa kwenda shule. Kufuatia mchango wa awali wa siku ya wakimbizi duniani, Shirika laAFRIpads na FARM STEW watafanya kazi pamoja kupitia ufuatiliaji wa mwisho wa utumiaji na tathmini juu ya athari za kutoa visodo vinavyoweza kutumika tena katika mipangilio ya wakimbizi pamoja na mtaala wa elimu.

Margaret Dipio, mkufunzi wa FARM STEW kwenye timu yetu ya uhamasishaji wa wakimbizi anaelezea thamani na matumizi ya AFRIpads kwa wasichana. Baadaye zaidi ya wasichana 200 walipokea vyao! 

Ili kuitambua siku ya Wakimbizi duniani, leo, mpango mpya wa; 'Hedhi Yako, Sauti Yako ' unatafuta kuwapa wanawake na wasichana wakimbizi fursa ya kusimamia hedhi zao kwa heshima. Mpango huo utazinduliwa Adjumani na wataona zaidi ya wasichana 200 waliohitimu umri wa kwenda shule ndani ya makazi ya wakimbizi. Boroli na Pagirinya wakipokea kifurushi cha AFRIpads chenye nguo za ndani, sabuni na kitabu cha elimu ya msichana.

'Hedhi yako, Sauti Yako ' itaanzishwa tarehe 20 Juni na miezi ijayo kuhusisha:

Mchango wa zaidi ya vifaa vya hedhi 900 vya AFRIpads (3 x maxi, 1 x super maxi visodo vinavyoweza kutumika tena). Elimu ya MHM na uhamasishaji kuvunja miko na unyanyapaa katika mada ya hedhi. Sehemu ya ufuatiliaji na tathmini ili kutathmini matokeo ya ushauri na ubora wa mpango-na kuhakikisha tunatoa sauti kwa wanawake wakimbizi na wasichana katika changamoto zao za MHM, mapendeleo na mahitaji. AFRIpads ni shirika la kibiashara la kijamii ambalo huwa na utaalamu katika utengenezaji wa visodo vinavyoweza kutumika tena vyenye gharama ndogo , usafi wa kike. Baada ya kufikia zaidi ya wanawake na wasichana 3,500,000 na vifaa vya hedhi vya AFRIpads, inaelewa kwamba kutoa suluhisho la bidhaa peke yake hakuwezi kushughulikia mahitaji tata ya wasichana na wanawake wakati wa hedhi.

Ufuatiliaji na tathmini ya mpango utatumia simu ya AFRIpads iliyojaribiwa na kupimwa ili kujenga uelevu  wa kina wa changamoto maalum za hedhi na mahitaji ya ndani ya makazi ya wakimbizi ya kaskazini mwa Uganda. Matokeo ya ripoti hii kisha yatalenga  kuongeza uelevu juu ya kiwango cha kimataifa na kuchangia data zilizopo ambazo zinajumuisha matokeo kutoka kwa utafiti wa majaribio katika 2018 na AFRIpads na UNHCR katika kusini Magharibi mwa Uganda.

Sarah Sullivan, Kiongozi wa Masoko na Mawasiliano wa AFRIpads, alisema:

"Zaidi  ya nusu ya ulimwengu wana uzoefu wa hedhi ,hata hivyo,wanawake na wasichana bado  wanakabiliwa na vikwazo visivyokuwa vya kawaida tu kwa sababu ya hedhi  zao. Hii hukasirisha zaidi hasa katika zaidi ndani ya mipangilio ya wakimbizi. Kwa matokeo, AFRIpads  inaheshimika kufanya kazi na Lunapads na Farm Stew katika kipindi cha usimamizi wa afya ya hedhi  ambao lengo lake  mahususi ni kuhakikisha  tunawapa wasichana wakimbizi na wanawake sauti zao kuonyesha kile wanachohitaji kusimamia hedhi  zao kwa heshima.

"Karibu miaka 10 ya uzoefu katika usafi wa hedhi imetufundisha kwamba, ili kuboresha jinsi wanawake na wasichana wanavyodhibiti hedhi yao, tunahitaji kutoa zaidi ya bidhaa tu. Uganda kwa sasa ni ya pili kwa ukubwa katika kuhifadhi wakimbizi duniani kote na pia nyumbani kwa kiwanda cha AFRIpads kwa hivyo tunatazamia kufanya kazi moja kwa moja na wanawake na wasichana wakimbizi katika mbinu hii ya afya ya hedhi."

Joy Kauffman, MPH, mwanzilishi wa FARM STEW ya kimataifa, alisema:

"Wanawake na wasichana wengi, kwa muda mrefu sana, hawajakuwa na njia ya heshima ya kudhibiti usafi wao wa hedhi. FARM STEW ya Uganda na ya kimataifa iko radhi kushirikiana na AFRIpads na Lunapads ili kutoa uhuru kutokana na aibu!

"Mpango wetu wa pamoja, 'Hedhi yako, Sauti yako ' itabadilisha maisha ya baadhi ya wanawake na wasichana wenye mazingira magumu. Kwa kusikia moja kwa moja kutoka kwa wakimbizi, tutakuwa na hakika kwamba aibu yao itaondolewa na heshima kurejeshwa. "

Lunapads, Shirika la Canada lililobobea kwa visodo vya hedhi vya kuosheka na nguo za ndani linafadhili mchango huu kupitia ushirikiano wao #One4Her na AFRIpads.

Jane Hope, msemaji wa Lunapads, alisema:

"Lunapads ina fahari kuleta visodo endelevu na vyenye heshima kwa mtu yeyote ambaye anahitaji. Hususan wakimbizi huwa na changamoto kupata  vifaa vya hedhi na kama kawaida, tunajivunia kushirikiana na AFRIpads katika kazi hii muhimu. "

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Joy Kauffman, MPH
Joy ni mwanzilishi mwenye shauku wa FARM STEW.
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.