Ilichapishwa
Novemba 22, 2019

Maji: Uhuru kutokana na Magonjwa na Kazi Ngumu

Joy Kauffman, MPH

 FARM STEW ilialikwa kwenye Kilima cha Wanyange, nchini Uganda, na Bi. Irene. Yeye ni mratibu wa kikundi cha wanawake wa eneo hilo.  Anapenda FARMSTEW na ashuhudia tofauti kubwa ambayo mafunzo hayo yamefanya katika jamii yake. Anasema,      

"Waume zetu walikuwa hata wakiteseka; hata walitaka kukimbia. Lakini sisi wanawake sasa tuko sawasawa; tuna bustani za jikoni za mboga, bustani za soya na tumejifunza kuhusu usafi wa mazingira. Kabla ya hapo,singeweza kunawa mikono yangu kamwe. Nilijua kuhusu sabuni lakini hatukuwa na  pesa  za kuinunua. Kisha tulijifunza kwamba tunaweza kunawa mikono yetu kwa kutumia majivu. Inatusaidia  kuwa na  afya.  Mungu aubariki mpango huu  hadi mwisho."

Kazi ya FARM STEW katika Wanyange ina matumaini sana, lakini bado hawana moja ya mambo muhimu ya maisha. Bi. Irene ni mmoja wa watu milioni 663 ambao hawana huduma ya maji safi. Pampu ya mkono katika kijiji chao ilivunja miaka iliyopita pamoja na asilimia 30 ya pampu zote barani Afrika.   

Bi Irene anaonyesha chanzo cha maji cha  kilima cha Wanyange.     

 Watu wanachota maji kwa ajili ya familia zao ambapo hatukuweza kufikiria kuyatumia kufanyia kitu chochote. Rangi ya matope ni dalili tu ya vimelea vinavyoishi ndani yake. Jionee mwenyewe hapa: 

Viini  katika maji machafu hufanya tumbo livimbe na bumba la minyoo ambayo hupata kula chakula cha kwanza kinapoingia matumboni mwa watoto. Muonekano wao ni wa kawaida sana: mikono ilyokonda, macho yaliyozama na matumbo makubwa manene ambayo yamejaa  maisha.

 Watoto wenye matumbo ya minyoo wanakula chakula cha Sabato mchana kanisani!  

Matokeo yake ni nini? Utapiamlo, magonjwa na kifo.

Hata hivyo, utafiti unaonyesha kwamba maji salama yanaweza kupunguza utapiamlo sugu kwa asilimia arubaini (40%) na kukosa kuhudhuria shule kwa asilimia thelathini (30%) au zaidi. Zaidi ya hayo, mapato ya nyumbani huongezeka kwa kiasi kikubwa (angalau 30%), wakati maji salama yanapotolewa, matumizi yanaweza kuelekezwa kutoka kwenye dawa na ada za kliniki zinazohusiana na magonjwa yanayotokana na maji hadi kwenye malengo ya uzalishaji.

Faida zilizopatikana kupitia upatikanaji wa maji salama sio tu kuboresha maisha na kupunguza umaskini  pia hutoa fursa kwa FARM STEW na Water4 na kuzima kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.

Jiunge na kampeni ya FARMSTEW kuhusu  Uhuru  kutokana na magonjwa na kazi ngumu  kwa kuchangia leo.

Bi. Irene, pamoja na Norah na wakufunzi wa FARM STEW wanaandaa chanzo cha ndani kwa matumaini ya hali ya maji. Aliandaa kikundi cha wanawake katika Klabu ya Akiba ya FARMSTEW, na sasa wana mboga za kuuza, kila mwanachama huleta Shilingi 6,000 za Uganda (kiasi cha dola 1.75) kila wiki.

Kwa msaada wako na wao, hali yao ya maji itabadilika katika miezi michache ijayo.

 Kikundi cha kuweka akiba cha FARM STEW cha Wanyange!  

FARM STEW imeshirikiana na Water4na wanawake hawa kuleta maji safi katika kijiji chao kwa kuhusisha kampuni ya uchimbaji ya mtaa iitwayo Freedom Drillers. Wanajamii watatakiwa kuleta mawe na mchanga na kufunzwa katika matengenezo ya kimsingi.   Akiba yao itatoa mpango wa bima wanaohitaji kuhakikisha kwamba pampu itaimarishwa na kutengenezwa haraka kama itawahi kuharibika!

Michango kwa FARM STEW itajumlishwa na Water4,  $1 kwa kila  $2 zilizotolewa, hadi $84,000!

Katika mwaka wa 2020 FARM STEW imepanga miradi 50 ya maji, kuwafikia takriban  familia 2,500 kwa gharama ya $15 kwa kila mtu kwa gharama ya wastani ya $4,680 kwa kurekebishwa au kuchimbwa kwa kisima. Tunahitaji kuongeza $150,000 ili kupata   ulinganisho wa $84,000. Msaada wako unahitajika leo!

Faida zilizopatikana kupitia upatikanaji wa maji salama haziboresha maisha na kupunguza umaskini tu pia zinatoa fursa kwa FARM STEW na Water4 ili kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.

Je, utachangia leo ili kusaidia kuleta maji safi kwa jamii kama kiima cha Wanyange? 

Pamoja na zawadi zenu leo, hivi karibuni, watoto watakunywa maji ambayo ni safi na wanaweza kujifunza juu ya chanzo cha maji ya uzima pia.

Chanzo cha maji safi kama hiki kimoja kitaboresha maisha ya  watu wote katika kilima cha Wanyange.

Je, utawasaidia kuleta maji kwao? Wasaidie watu kumi kwa  $150 leo, bonyeza hapa!

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Joy Kauffman, MPH
Joy ni mwanzilishi mwenye shauku wa FARM STEW.
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.