Kumi bora kutoka mwaka 2017
Waliokuwa 10 bora wa FARM STEW mwaka 2017
Kuangalia nyuma katika mwaka wa 2017, Nasimama nikishangaa.
Mungu amekuza FARM STEW kutoka mche unaochipuka mpaka mmea uliokomaa ambao unazaa matunda! Shukran. Inathibitika kuwa ya kudumu! Ninawaalika kushiriki "mmea" wa mwaka uliopita ilihali tukielekeza mawazo yetu kwa kazi ya mwaka 2018.
10. Tunaelezea ujumbe wa FARM STEW katika vyuo vikuu 3, makanisa na mikutano katika majimbo 5!
9. Kufikia mwisho wa mwaka, FARM STEW ilikuwa na wafanyakazi 8 wa kudumu waliopelekwa Uganda kufundisha mafunzo kuhusu maisha tele.
8. Tulijumuisha vyakula vya kitropiki na vya kienyeji katika madarasa ya upishi.
7. Wanafunzi wawili wa ngazi ya shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Andrews waliwahi kuhudumu kama wanagenzi na walikuwa na mtunza vitabu wa kujitolea, mbunifu wa picha, Meneja wa teknolojia ya habari, na wa kujitolea wengine, wakiteremsha gharama zetu za msingi za Marekani.
6. Tulikuwa na wafadhili 152 katika mwaka wa 2017 ikilinganishwa na 10 tu katika mwaka wa 2016!
5. Timu yetu ya Uganda ya mafunzo katika magereza na nyumba za yatima, mashirika yanayofanya kazi na watoto wa mitaani na waathirika wa VVU/UKIMWI.
4. Timu yetu yote ya kujitolea ya FARM STEW ya Zimbabwe yaongoza mafunzo katika vijiji kadhaa na makao ya watoto yatima.
3. Tulianzisha kundi letu la pili la FARM STEW Uganda lililoko Jinja, chanzo cha mto Nile.
2. Takriban wasichana 1,000 wana uhuru kutokana na aibu, shukrani kwa visodo vinavyofuliwa.
1. Katika mwaka wa 2017 peke yake, FARM STEW ilifundisha wanakijiji 13,122 wa Uganda (theluthi mbili za wanawake) kwa muda wa jumla ya masaa 1,984. Hii huleta jumla ya masaa yote kuwa 25,319 ya mafundisho.
Zaidi ya takwimu yoyote au ukweli, FARM STEW ni kuhusu kupatikana kwa elimu rahisi ambayo inaweza kuokoa maisha, kufunzwa na kujifunza kiutendaji na wenyeji! Phionah (aliye upande wa mwisho wa kushoto) mkufunzi wa FARM STEW wa Uganda alimuhoji Idha (aliye upande wa kulia), mama wa watoto 10 mwenye umri wa miaka 43, baada ya siku ya tatu ya mafunzo katika kijiji chake. Napenda kile alichosimulia!

"Nilitaka kujua njia bora ya kuwalisha.Kama mama,Nilihisi kuhukumika kwa kutowatunza vyema watoto wangu lakini sasa sina hisia za hukumu tena... Naamini kama kila mtu ataweka katika mazoezi kile FARM STEW inachofundisha, wanaweza kuboresha afya zao kama mimi ninavyoanza kuona kwa watoto wangu. Mungu awabariki (FARM STEW) munapoendelea kuja kutoa mafunzo kwetu. "
Tafadhali saidia kufundisha kichocheo cha maisha tele!