Kuchelewa mno kwa Jovia
Jennifer, mamake Jovia, alikumbatia ujumbe wa FARM STEW. Mkufunzi wetu, Dan Bautama (katika kijani) alianza kufanya kazi katika jamii yake ya vijijini Mashariki mwa Uganda miezi michache iliyopita. Kwanza alilenga sana juu ya "usafi" wakati alitambua kwamba kulikuwa na vyoo vichache sana na hakukuwa na vituo vya kuosha mikono. Watoto wenye kutokwa na kamasi puani wanahakikisha jambo hili.
Shukrani kwa msaada wako, wakati Joy alipowasili mwezi Mei, mabomba ya mifereji yalikuwa kila mahali na jamii ilifanya maendeleo mengi. Walikuwa na furaha kushiriki yote waliyokuwa wamejifunza!
Jennifer alipenda bomba lake la mfereji sana kwamba nilimuonyesha akinawa mikono katika ukurasa wetu mpya wa Masomo ya kimtandao ya kujifunza nyumbani. Niliangalia picha hii mara nyingi wakati huu wa majira ya joto kama tunavyojiandaa kwa bidii kwamba siku moja itabariki mamilioni (tunatumaini) na kichocheo cha FARM STEW cha maisha tele.

Nililia mwezi uliopita nilipopokea habari hii kutoka kwa Dan:
"Habari Bi. Joy , kwa huzuni kubwa natangaza kifo cha mtoto wetu mpendwa kutoka kikundi cha FARM STEW cha Buwambiidhi. Natumai unakumbuka mtoto huyo wakati tulipotembelea kijiji hicho katika mashamba ya miwa. Tulikuwa tumekuja kwa mafunzo leo, kwa bahati mbaya, tulikumbana na habari za huzuni, sasa tunahudhuria mazishi. "
Mbona ninatoa machozi hata sasa?
Kitakwimu, Jovia ni mmoja wa mamilioni, lakini kifo chake kilikuwa cha kipekee kwa familia yetu ya FARM STEW na kwangu. Baada ya miezi michache ya mafunzo ya FARM STEW katika jamii ya Buwambiidhi Mashariki mwa Uganda, bustani ndogo za jikoni zilikuwa zimeanza kuzalisha chakula. Wanakijiji walilima kwa bidii maeneo yazungukayo nyumba zao.


Cha kusikitisha, kama unavyoona hapo juu, mengi ya yale tuliyofundisha kuhusu "ukulima,"ingawa hayakuweza kutekelezwa ni kwa sababu shamba linalozunguka kijiji lilikuwa limetengewa upanzi wa miwa badala ya vyakula vya virutubishi vingi. Mikataba ya miaka mingi kutoka makampuni ya kimataifa huleta majaribu kwa watu maskini lakini huishia kupata hasara zaidi kuliko faida.
Hiyo ndiyo sababu mafunzo yetu ya "Ujasiriamali" ni muhimu sana!
Nilipokutana na Jennifer, mara moja nilikuwa na wasiwasi na nywele za mtoto wake Jovia. Sehemu nyekundu za viraka vya nywele zilizokunjana zilibaini mtoto aliyekuwa na utapiamlo sana. Nilimwambia Dan atusaidie kuzungumzia jambo hili. Baada ya kujifunza kwamba Jennifer alikuwa akimlisha Jovia uji wa mahindi sana, nilidhani Jovia alikuwa akikosa protini, madini ya chuma, vitamini C ambayo ingesaidia kunyonya madini ya chuma na pia vitamini B.

Jennifer alisita kiasi kwa sababu hakuweza kufikiria kwamba mtoto wake mdogo mnene Jovia angeweza kuwa na utapiamlo. " Si ukubwa wake unaashiria malezi yangu mazuri kama mama?" alionekana kushangaa.
Tulipendekeza kwamba Jovia alihitaji kwenda katika uchunguzi wa kimatibabu.Tulimpa Jennifer ushauri wa kunyonyesha kama inavyohitajika na kuanza kumlisha Jovia aina mbalimbali za vyakula vya kupikwa na kupondwa vinavyopatikana kienyeji. Dan alirudi muda mfupi baadaye na kuanza upanzi wa miche ya mboga. Alilenga sana juu ya lishe, mafunzo ya "chakula" chetu.
Lakini Jovia alikuwa amechelewa sana. Jovia alipata malaria na kufariki kwa sababu ya upungufu wa damu ambao ni ukosefu wa madini ya chuma.
Biblia inasema kwamba "Uhai wa mwili uko katika damu" (Mambo ya Walawi 17:13) na ni kweli. Bila ya madini ya chuma, chembechembe zako nyekundu za damu haziwezi kutoa oksijeni kwa mwili wako na chembechembe zako kwa kweli hukosa hewa. Hivyo ndivyo ilitokea kwa Jovia.
FARM STEW imeundwa ili kushughulikia ukweli unaovunja moyo kwamba katika Afrika ya Kusini mwa jangwa la Sahara, watoto 5 wenye umri wa chini ya miaka 5 hufa kila dakika. Wengi hawana majina na vifo vyao havitagusa maisha yetu lakini Jovia ni tofauti. Tunafahamu kisa chake na jina lake.
Ndiyo maana tumeweka wakfu Masomo yetu ya mtandao ya kozi ya FARM STEW kwa kumbukumbu yake.