Matokeo mabaya ya sukari
Sukari,katika hali yake safi nyeupe na fuwele huonekana bila madhara lakini sisi sote tunakubaliana kwamba ikiwa nyingi inaweza kusababisha mianya kwenye meno na kuongeza uzito zaidi. Hata hivyo, meno yetu huitamani na mahitaji yake ulimwenguni hayajawahi kupanda. Hata hivyo, katika njia ambazo huenda usiifikirie, ina madhara makubwa kwa watoto.
Je umewahi kuona ukikua? Muwa hukua wima na kwa urefu. Ni aina ya mti wa kudumu unaostawi katika hali ya hewa ya kitropiki, zao la kuuzwa, linalokuzwa na makampuni mengi ya kimataifa katika nchi maskini. Katika hali ya kejeli mbaya, miwa ni sehemu ya kisa kinachosababisha milioni 58,000,000 ya watoto wa kiafrika kuwa na ufupi wa uliokithiri na matokeo mabaya yasioweza kugeuzwa
Je, watoto wafupi wanahusikanaje na miwa? Je, wote wanaweza kuchangiaje umaskini? Ili kujua, ninawaalika kuja katikakijiji cha Wagona, mashariki mwa Uganda.
Paa la umaskini na vibanda vya matope vilivyotawanyika katika njia nyembamba zilizofunikwa na kivuli cha mashina ya miwa. Wakati makampuni makubwa yalipohama muongo mmoja uliopita, wanakijiji wengi waliacha kukuza mazao yenye virutubishi vingi kama vile mtama na kunde kwenye mashamba yao madogo. Wanakijiji walibadili chakula kwa ajili ya ahadi ya fedha.
Robert, mtaalamu wa kilimo wa Farm Stew Uganda , anaarifu kwamba "familia nyingi zinakosa chakula kwa sababu nchi yote inatumika kwa ajili ya kukuza miwa ya sukari badala ya kukuza chakula. Watoto hupatwa na magonjwa ya lishe na afya mbaya ya familia kwa ujumla. "
Kwa muda, thamani ya miwa imepungua kwa kiasi kikubwa kwenye soko la wenyeji. "Mazao ya kuuzwa" yanaweza kuwaacha familia kuwa na umaskini uliokithiri! Ni mzunguko mbaya na watoto wanakabiliwa vibaya zaidi ya yote.
Nashukuru, kupitia zawadi zako,FARM STEW inatoa suluhisho!
FARM STEW iliendesha mafunzo yake ya kwanza huko Wagona na washiriki 55, tarehe 23 Januari 2018. Mafunzo ya ziada ya vikao vya kiutendaji ya siku mbili yalifanyika katika wiki zilizofuata, ambapo watu 88 walishiriki kikamilifu. Kwa kufundisha viungo vinane vya kichocheo cha maisha tele vya FARM STEW (Ukulima, Mtazamo, Mapumziko, Chakula, Pumziko, Usafi, Ujasiriamali, Maji)tunaziandaa familia hizi kuvunja mzunguko wa umaskini, kuwahimiza kurudi kwa maadili ya chakula cha kinyumbani na kiwanda cha kienyeji.
Mwezi uliopita, Robert, (mwenye mavazi ya kijani), alitumia wakati na wakazi wa Wagona, David na mkewe Fatuma wakati wa moja ya ziara nyingi za nyumbani za FARM STEW katika jamii. Robert alivutiwa sana na bustani yao mpya iliyostawi. David, Fatuma na familia nyingine nyingi, walionyesha matokeo ya mbinu walizojifunza kutoka kwa FARM STEW.
Kwa furaha, Fatuma alisema, "Kabla ya kuja kwenu, fedha kidogo mume wangu alizopata kama mshona viatu hazikutosha kulisha familia na kulipa karo za shule kwa ajili ya watoto wetu wanane. Niliogopa kulima (kilimo) kwani nilifikiri ilikuwa ni laana. "
Hisia hiyo ya huzuni ni ya kawaida tu. Watu wengi wanaamini kuwa bustani ya mboga ni zaidi ya uwezo wao na chini ya heshima yao. Kwa $15 tu kwa kila familia $150) kwa 10, tunaweza kushinda kikwazo na kuwasaidia kuanza bustani.
FARM STEW inawakumbusha wanakijiji ukweli rahisi wa kibiblia kwamba tuliumbwa katika bustani na kuambiwa tuitunza. (Mwanzo 2:8, 15) wakati huo, hakukuwa na laana na Mungu alitangaza kila kitu kilikuwa "kizuri sana!"
Kupitia kwa usaidizi wako wa ukarimu, tunaweza kuwafikia watu ambao ni miongoni mwa maskini na wenye njaa zaidi duniani. Tunawakumbusha kwamba watu wa Mungu walikuwa ni wakimbizi na maskini sana. Mungu alituma ujumbe kupitia nabii Yeremia (29:5) kwa watu wake akisema, ""Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake."
David na Fatuma walijifunza kwa dhati! Alielezea, "baada ya FARFM STEW kutufundisha manufaa ya bustani na kutupa mbegu za mboga, ilinibadilisha maisha yangu. Sasa ninajiona kama mtu muhimu sana katika jamii yangu. Kwa kupanda mboga, tuna uwezo wa kuziandaa na kula na zimetuboredha afya yetu. Baadhi ya watu katika jamii sasa huja kununua mboga. Sasa nina mboga katika hatua zote za ukuaji; katika kitalu, na zile ambazo zimekua na zilizo tayari kuvunwa. Kwa kuuza za ziada, sasa ninaweza kupeleka watoto wangu shule na kuangalia mahitaji ya msingi ya nyumbani, hivyo kumsaidia mume wangu."

Wanandoa hawa wenye furaha, wananikumbusha juu ya ukweli rahisi ambao FARM STEW inazingatia, "wakati mbinu sahihi za kilimo zinapotumika, umasikini utapungua sana kuliko ulivyo sasa. Tunakusudia kuwapa watu mafunzo ya utendaji juu ya kuimarika kwa nchi, na hivyo kusababisha kulima ardhi yao, ambayo haitumiki kwa sasa.
Tukikamilisha hili, tutakuwa tumefanya kazi nzuri ya utume. " (EGW, barua 42, 1895)
Hongera kwa kazi yako nzuri, lakini kisha pumua kwa kina kwa kuwa kuna kazi nyingi za kufanywa bado. Turudie watoto wafupi, sukari na umaskini, Je, wana kitu gani sawiya wote? Kwa neno moja tu, utapiamlo.
Watoto hawa wa kiafrika wenye umri wa miaka 9 wanaweza wasionekane kuwa watapiamlo. Unaweza kufikiria ni wafupi. Nani anayejali? Lakini ni wakati gani ufupi ulikuwa kitu kibaya?

Jibu ni, kudumaa, hufafanuliwa kama urefu kwa umri ulio chini ya kawaida. Huwezi tu kuangalia watoto na kujua kama wamedumaa lakini bado ni aina ya utapiamlo iliyo mbaya zaidi .
Kama aina nyingine za utapiamlo, madhara ya kudumaa hayabadiliki. Athari zake hujumlisha ukosefu wa uwezo wa kujifunza, ukosefu mbaya wa mafanikio, hatimaye upungufu wa uzalishaji, afya mbaya na unene kupita kiasi.
Ndio maana kuzuia ni muhimu na kwa nini Farm Stew inalenga familia na ujumbe wa ukamilifu. Sababu za kudumaa ni lishe duni na maambukizi yanayojirudia hasa katika siku 1,000 za kwanza za maisha. Muda mfupi, kutoka utunzi wa mimba hadi miaka miwili, huamua mustakabali wao.
Je, hiyo inahusianaje na sukari? inanishawishi pamoja na timu zetu.
Nilipokuwa nchini Uganda miezi michache iliyopita, mimi na Julius, mmoja wa wakufunzi wa FARM STEW, tulikuwa tukitembea kupitia maeneo ya miwa kuelekea kijiji ambacho tulikuwa tunafanya mawasiliano ya kwanza. Njiani tulimkuta kijana huyu mdogo aliyekuwa akilia akiwa amekaa chini ya tonobari la plastiki na kitu kidogo cheupe katika mkono wake.
Tulijua jina lake, Yusufu, na kwamba mama yake alikuwa amefariki. Wakati baba yake alikuwa akifanya kazi katika mashamba ya sukari,
Aliachwa siku nzima na kitita cha miwa atafune. Nilivunjika moyo, lakini baadaye katika maombi, alinitia nguvu kupitia aya hii.
"Tena tusichoke katika kutenda mema, maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho." Wagalatia 6:9

Watoto wengi kama Joseph wanateseka kutokana na njaa, magonjwa na umaskini. Hawapati kile ambacho miili yao michanga inachohitaji ili ikue. Shauku ya FARM STEW ni kuwafikia. Uchaguzi wako wa kufanya vyema, kupitia zawadi yako, inaruhusu timu zetukutokufa moyo!
Mimi nimebarikiwa sana kwamba umechagua kufanya uwezekano wa kuwafikia watu 34,295 na mafunzo yetu hadi sasa. Wito unakuja kutoka vijiji vingi. Tuna mtumaini Mungu, lakini ni juu yenu kufanya iwezekane.
Kichocheo cha maisha tele, kimejengwa juu ya msingi wa sayansi ya kuthibitika, miongo ya utafiti katika maendeleo ya kimataifa na Biblia. Matokeo yake ni kwamba maisha yanabadilishwa kimwili, kiakili na kiroho. Je unaweza kusaidia kupanua na kuimarisha tuwafikie watu zaidi?
Nina uhakika kuwa maisha ya Joseph bado ni magumu lakini majuma machache baada ya tukio hili, timu yetu ya FARM STEW iliweza kurudi katika kijiji chake kuwapa mafunzo wenyeji kuhusu vyakula vya virutubishi vidogo ambavyo wanaweza kumudu kuvitengeneza na kuwapa watoto kama yeye. Tukiongozwa na Yesu, masomo yetu huhimiza wenyeji kuwa na huruma kwa wadogo kati ya hawa kama Joseph.
Nimetiwa moyo sana na visa vya familia za Uganda ambazo zinawafikia watoto kama Joseph. Kwa mfano, huko Jinja, Uganda tumekuwa na mafunzo katika makao ya nyumba za mayatima zinazosimamiwa na wenyeji. Ni watu waliosadiki mwito wao wa kujali
Mwanamke mmoja kwa jina la Samara ana watoto 60 wenye matatizo ya kukua katika nyumba yake. Anashangazwa na walivyo bora kwa chakula kipya cha bei nafuu na mabadiliko rahisi katika usafi na mtazamo. Yeye pamoja na asilimia themanini (80%) ya wale wote waliofanyiwa utafiti wanaipa heko Farm Stew kwa kazi nzuri yenye athari muhimu katika maisha yao.
Je, utaendelea kushirikiana na watu kama vile Samara ili kufikia watoto kabla wadumae?