Soya na mboga kwa ajili ya amani?
Najaribu nisiwe mtu wa kuigiza lakini kwa kweli, hii ni suala la kifo na maisha, vita na amani.
Nimerejea tu kutoka Afrika, ambapo mdundo wa moyo wa FARM STEW hupiga kwa nguvu. Wakufunzi wetu wa Kikristo wanafanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi ili kuwafikia watu. Wanahitaji virutubishi viwili muhimu mbili, fedha na sala. Zawadi zenu ni uhai wa maisha ya huduma hii. Shukrani kwako, athari yetu inaongezeka kila siku. Maombi yangu ni kwamba zawadi zako ziendelee kutiririka.
Ningeweza kuandika kitabu kifupi juu ya visa vya watu ambao walionyesha matumaini yao kwa siku za usoni kama matokeo ya pekee ya kufanya uwekezaji wetu katika FARM STEW. Leo hii, nitazungumzia wachache tu kutoka kwenye kambi za wakimbizi kaskazini mwa Uganda ambako timu yetu ya Sudani Kusini ya kuwafikia ilizinduliwa mwezi Machi mwaka wa 2018.
Joseph Malish, mkimbizi kutoka Sudani Kusini na mzee wa Kanisa, ni mkufunzi wa FARM STEW huko. Kama wengine wengi katika Biblia, alipewa jina jipya, "Malish Leben." Leben inamaanisha "maziwa" kwa Kiarabu, lugha ya kawaida miongoni mwa makundi mengi ya kikabila.
Tendo rahisi la kubadilisha soya kuwa maziwa ni jambo la kushangaza kwa wakimbizi wenzake, kwamba imekuwa muhimu kwa utambulisho wake. Wanaipenda na wanampenda! Kwa kushangaza, "Malish Leben" anaamini kuwa maziwa haya ya msingi yanaweza kuwa ufunguo wa kumaliza mapigano baina ya makabila. Hiyo inaonekana kuwa ni ajabu, najua, lakini inaweza kuwa kweli.
Sikiliza jinsi Elias ameshawishika na wazo hilo hilo katika video hii fupi:
Lakini ulimwengu bado haujajua matumaini ya FARM STEW!
Redio ya Kitaifa ya kutangaza (NPR) ilitoa kisa cha kuvutia mwezi wa Novemba ambapo ilisema, "Sudan Kusini ina moja ya mgogoro mkubwa wa wakimbizi duniani hivi sasa ... Aina ya fedha inayopendelewa ya Sudani ya Kusini sio fedha, bali ni ng'ombe. "Vurugu nyingi ni juu ya wizi na mauaji ya ng'ombe.
Kuua watu kwa ajili ya ng'ombe imekuwa kawaida katika nchi ya Sudan Kusini. Joseph alielezea jinsi makabila ya Nuer na Dinka ambao hasa wanapenda maziwa ndio maadui waovu zaidi.
Katika mafunzo ya FARM STEW, makabila arubaini na mawili huja pamoja, ikiwemo Nuer na Dinka. Joseph alielezea mafunzo ambapo watu arubaini na watano walihudhuria kutoka makabila mengi tofauti. Ingawa anazungumza lugha nyingi, alimwomba Mnuer kutafsiri kwa Mdinka. Wakati wa mafunzo ya masaa manane, kikundi kiliunganika pamoja kupitia kazi yao ya pamoja ya maandalizi ya chakula. Mwishoni walikaa pamoja kula lishe bora, vyakula vya kienyeji kutoka kwenye vyungu vya kawaida na kunywa maziwa kutokana na soya ya kawaida. Washiriki walisema walitaka kuja kila siku kujifunza zaidi. Je, unaweza kuona jinsi ujumbe huu unavyoweza kusaidia katika kuzilainisha nyoyo?
Ripoti kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo lakisia kuwa, "kiasi cha asilimia themanini (80%) ya idadi ya watu wa Sudan Kusini hutegemea mifugo kwa kiwango fulani. Kwa makundi mengi: vijana, kina mama wanaonyonyesha na wafugaji ni chanzo chao Kikuu cha lishe. " Lakini wakati wanalazimika kukimbia kama wakimbizi, ng'ombe wote wanauawa au kuachwa nyuma. Joseph "Malish Leben" anatabiri kwamba uwezo wa wakimbizi kutengeneza maziwa yao inaweza kuwa ufunguo wa uponyaji kwa taifa lake.
Mwandishi wa NPR alimwuliza mkaazi ambaye ng'ombe wake walikuwa wameibwa: "Je, unafikiriaje maisha yako ya baadaye bila ya ng'ombe?" Jibu lake kupitia kwa mkalimani lilikuwa: "Nafikiri nitaishi maisha ya matatizo sana. Maisha bila ng'ombe ni kama ambaye hakuna uhai. " Ndio maana kwa kiasi wakimbizi wengi hushikwa na majonzi.
Maneno yake yananikumbusha juu ya nusu ya kwanza ya fungu la mada ya FARM STEW, Yohana 10:10,
"Mwizi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu." Vitenzi hivyo vitatu vya kutisha vinatoa muhtasari wa historia ya Sudani ya Kusini.
Yesu ndiye jibu. Anakuja, "ili tupate uzima, na tuwe nao tele." Huo ndio utume wa FARM STEW na inatumika kama mkono wa kuume wa injili!
Hitimisho la kisa cha NPR linasema, "wanamwambia hakutakuwa na amani bila matumaini kwa siku zijazo. Na katika Sudani Kusini, matumaini yake ni ya kupiga kwato. "
FARM STEW inaweza kuwafunza watu kukuza tumaini kwa njia ya maharagwe ya soya rahisi na kujifunza matumaini yetu ya kweli katika Yesu!!
Njia nyingine ambayo tunaleta matumaini kwa wakimbizi ni kwa kutoa visodo kwa wasichana. Tayari tumetoa visodo kwa wasichana wakimbizi 89 mwaka huu katika shule ya Waadventista ya Pagirinya. Wasichana hawa ni akina mama wa siku za usoni na kwa muda mrefu wao hukaa shuleni,ambavyo ni vizuri. Utafiti unaonyesha kwamba viashiria vyote vya afya ya mtoto vinahusiana na elimu ya mama. Unapotuma tu $10 kwa msichana, kuruhusu FARM STEW kuwaandaa kwa usafi wa hedhi, unaweza kuathiri vizazi vijavyo. Tunataka kufikia wasichana 2,018 mwaka huu, tunahitaji $14,750 zaidi kufikia lengo hilo!
Unaweza kuona sasa kwa nini hili ni suala la maisha na kifo? Zawadi zako za kuhamasisha wakufunzi wa FARM STEW na kufikia mahitaji ya kimsingi ya wasichana zinaokoa maisha sasa na baadaye.
Kazi katika kambi za wakimbizi imeanza sasa. Mwaka jana wakati kama huu tulikuwa na wakufunzi wa wakati wote wa Kiafrika, na kwa imani sasa tumesambaza wakufunzi kumi na saba katika timu nne zetu kote Afrika! Tunahitaji msaada wako kusambaza ujumbe zaidi na kusitisha makabila yanayopigana! Je, utatuma zawadi ya ukarimu leo? Tunahitaji kuhamasisha wakufunzi na kuandaa wasichana!
Pamoja na zawadi zenu tunawasaidia wakulima kukuza maisha yao na ya baadaye. Kuna kisa kimoja cha mwisho hapa!
Doreen Arkangelo, kiongozi wetu Sudan Kusini wa timu ya kufikia pia ana jina jipya. Amekuwa kiongozi wa Kanisa katika idara ya wanawake na maisha ya familia kwa miongo kadhaa. Sasa anaitwa "mama Geregere," maana "mama wa upinde wa mvua" katika lugha ya Kimari. FARM STEW yahimiza nguvu ya kula lishe kamili na upinde wa matunda na mboga za kienyeji kwa ajili ya afya. Umuhimu wake haujawahi kuwa juu kama ulivyo katika kambi za wakimbizi ambapo mazao safi ni nadra sana.
Sheria ya ugavi na mahitaji hutufundisha kwamba kile ambacho ni nadra ni cha thamani.
Hiyo inaweza kuwa baraka kwa wakimbizi waliopewa mafunzo ya FARM STEW na wako tayari kufanya kazi kwa bidii kama Francis, mkimbizi, mzee wa Kanisa na baba wa wa watoto sita na mwenye kutunza yatima. Kuwapa watu kama Francis njia ya kuendeleza familia yake ni furaha yetu.
Pamoja na mama Geregere, tulikwenda kwenye uwanja nje ya kambi ya wakimbizi ambayo Francis amekodisha kutoka kwa Mganda mwenyeji. Iko chini na mbali na "barabara" ambayo haipaswi kuwa na muundo huo. Mahali "barabara" ilipoishia tulitembea nusu maili nyingine. Vibanda vya matope tulivyopita njiani vilikuwa na watoto wengi waliokonda na matumbo makubwa yakiwa na uwezekano wa kuwa na minyoo. Wanawake walikuwa wakianika mihogo (mmea wa mzizi wenye wanga) kwenye mkeka juani ikiwa katika hatua tofauti tofauti za kutengeneza pombe. Ilikuwa ni huzuni.
Kinyume na matarajio, ilikuwa ni furaha kufika katika shamba la Francis la soya na mboga. FARM STEW ilitoa mbegu na mafunzo miezi michache iliyopita. Safu nzuri na matandazo ya kutosha ilionyesha kuwa Francis alitumia ujuzi vizuri. Mkondo mdogo wa mto uliopo robo maili nyingine chini ya kilima ilikuwa chanzo chake cha maji ya kubeba kwa mkono ili kukuza ukuaji. Alitengeneza hali ya hewa iliyofanya mbegu kustawi na kufanya kazi. Mimea ya soya ilikuwa inakaribia wakati wa mavuno, pamoja maganda ya manjano yaliyonenepa na kufunika shina la katikati la mti. Mapaa ya miche ya mboga za kitalu iliyo na afya kamili zenye urefu wa nchi moja, zilileta matumaini! Miche italeta afya na uzima badala ya kifo cha pombe rahisi ya muhogo.
Francis alieleza kwamba hivi karibuni alikuwa amevuna nyanya nyingi. Ilikuwa ni ajabu kusikia kile alichofanya na faida aliyopata. Akiwa mkimbizi mnyenyekevu ambaye sasa ni mkulima mwenye ujasiri, alinielezea kwamba aliweza kuwapeleka watoto wake kwenye shule ya Kikristo. Hata kama shule imejengwa kwa vijiti na madarasa yametengwa kwa kutumia karatasi nyeusi ya plastiki kama ile inayotumika katika mikebe ya takataka, Francis anafurahia katika maisha ya baadaye ya watoto wake.

FRANCIS amepata motisha sana kwa mafanikio yake.
Zawadi zako kwa FARM STEW pamoja na bidii yake ilifanya iwezekane!
Ingawaje shauku yao kwa Bwana iko karibu, hawa wakimbizi, wanakabiliwa na changamoto ya kila siku ili kuyalinda maisha. Ndio maana tuliendesha mpango wa mafunzo ya kina ya wakufunzi ili kuongeza maarifa na ujuzi wao wakati wa mkutano wao wa makambi. Wakufunzi wetu kumi na watatu wa FARM STEW wa kiafrika wanaoishi Uganda waliungana na wakimbizi kumi ambao wanahudumu kama watu wanaojitolea. Tulipiga kambi katika mahema chini ya anga iliyojawa na nyota na kulala tukisikiza kwaya za vijana wa makambi ambayo tulialikwa.
Tulifanya mazoezi mara kadhaa kwa siku ya kile tulichojifunza kwa kuwafunza wakimbizi elfu waliokusanyika katika makundi chini ya miti mbalimbali waliogawanyika kwa muda mfupi kilugha. Ilinikumbusha sana juu ya amri ya kuhubiri kwa mataifa yote, makabila, na lugha. Kicheko kilipita lugha na kunena kwa sauti kuhusu maisha!
Thomas Amoli, mchungaji wa makanisa ya mitaa, mtetezi imara wa FARM STEW, alielezea kiwewe kikali cha wakimbizi. Alielezea kwamba kazi katika kambi zinaweza kuwa kubwa lakini kwamba FARM STEW imekuja kwa wakati ufaao tu. "Moses na Joshua, hii ni kama huduma ya Kanisa na FARM STEW," alisema mchungaji Amoli.
"Nimefurahi sana na FARM STEW kwa sababu ni mkono wa kuume kwa wakati mwafaka wa huduma."
Mchungaji Amoli alishuhudia ukweli kwamba kazi ya FARM STEW inaleta uhai katika makanisa!
Mungu anafungua milango mingi kwa ajili yetu ili kuelezea kuhusu kichocheo cha maisha tele lakini wakati ni mfupi! Milango itafungwa kwa haraka kama ilivyofunguliwa kwa sasa. Vurugu za mauaji siku chache tu kabla ya kuwasili kwetu ilisababisha viongozi kutuzuia kuingia katika kambi moja ambapo tuna wakufunzi wawili wa FARM STEW. Sababu pekee inayowawezesha kuendelea kufanya kazi ni kwamba ni wakimbizi waliosajiliwa kama wakaazi katika kambi hiyo. Ndio maana ni muhimu sana kuwafundisha washiriki wetu wa Kanisa katika kambi hizi! Na hao ndio mitume wanaoleta habari njema.
Pamoja, lazima tuchukue hatua kwa haraka ili kuelezea kuhusu kichocheo cha maisha tele -- FARM STEW!
Nina mengi zaidi ya kuelezea, kwa hiyo tarajia barua pepe zinazokuja kutoka kwangu katika majuma yajayo. Tafadhali omba! Ninaamini Bwana atakuongoza kwa sharti la ukarimu kwa sababu naamini kazi hii iko katikati ya mapenzi yake.
Msaada wako endelevu utaenda kutia uhai FARM STEW
