Wakimbizi wapambana na dhana potovu za hedhi
Makala hii ilionekana katika New Vision, Gazeti linaloongoza la Uganda
Margaret Dipio wa miaka 43 aliondoka Sudani Kusini mwaka 2014 na aliwekwa katika makazi ya wakimbizi ya Boroli katika wilaya ya Adjumani kaskazini mwa Uganda. Kwa kuishi miongoni mwa watu wenye asili tofauti ya utamaduni, hivi karibuni, Dipio alitambua mitazamo mbalimbali ya kikabila kuhusu hedhi. Moja ya mitazamo ambayo amekumbana nayo ni kwamba kipindi cha hedhi ni hali iliyona kasoro kibaolojia, kwa hivyo msichana hutengwa kila mwezi anapopata hedhi. Msichana hatarajiwi kugusa chombo chochote cha kupikia licha ya kumsalimia mtu yeyote.
Kwa ujumla, yeye huonekana kuwa mchafu na mbaya zaidi ya wote hasa kama hedhi zake zinakuja na maumivu, huhusishwa na laana ya mababu. Katika makazi ya Boroli, baadhi ya tamaduni huaminika kwamba msichana katika kipindi chake lazima huwa na shimo sawa na ukubwa wa sehemu yake ya nyuma, ambayo hutarajiwa kukaa kwa masiku bila kuoga mpaka hedhi yake iishe.
Imani hizo hapo juu zaonyesha kwamba hakuna mtu anayepaswa kuigusa damu ya hedhi inayotoka hasa isije ikasababisha huyo msichana kuwa tasa baadaye. Kwa hiyo, mikakati mikali imewekwa ili kuzuia hili kutokea. Hicho ni kiwango cha hadithi za kizamani za jadi juu ya hedhi ambazo Dipio na wengine wachache wako nje ili kukabiliana kati ya chuki kali kutoka sehemu ya Kihafidhina ya jamii yake.
Wakiwa na tumaini dogo la mafanikio, Dipio na wengine walianza kuzungumza na viongozi wenye ushawishi na wa kidini kuhusu hitaji la msururu huu wa mawazo finyu kuhusu hedhi. Kikundi hicho kilitembelea shule na makanisa ili kuzungumzia usafi wa hedhi pamoja na kusisitiza haja ya jamii kuacha mila ambazo zinawarudisha nyuma wanawake katika makazi ya wakimbizi wa Boroli na ulimwenguni kote
"Baadhi ya wanawake wanaogopa kuwaambia waume zao kuhusu kuwanunulia visodo wasichana wao," Dipio alisema.

[Dipio ni mkufunzi wa FARM STEW Uganda, Shirika la Taifa lisilo la kiserikali pamoja na huduma ya kuboresha afya na ustawi wa familia maskini na watu walio katika mazingira magumu.]
"Wakati tunapokuja pamoja kukuza mboga, pia tunazungumzia kuhusu shida za wanawake katika jamii yetu," Dipio alisema. Wanatembelea shule za msingi katika eneo hilo kulenga wasichana hasa watano hadi saba kuzungumza nao kuhusu usafi wa hedhi.
Dipio pia anatoa mafunzo kwa wasichana kuhusu matumizi sahihi ya visodo. Anasema kuwa ujumbe wao unaingia taratibu katika kujaza upungufu unaoletwa na vikwazo vya utamaduni katika jamii "Wengi wanaacha tabia hiyo mbaya polepole," alisema.
Hata hivyo, vita vyao dhidi ya ubaguzi unaohusiana na hedhi, vinazuiwa na umaskini wa nyumbani katika makazi ya wakimbizi.
"Baadhi ya familia haziwezi kujimudu kununua visodo kwa ajili ya binti zao," Dipio alisema.
Katika shule ya msingi ya Boroli, mwalimu mkuu wa kike, Harriet Walea, alisema wasichana, hasa kutoka katika makazi ya muda huwa na uwezekano wa kukosa masomo wakati wanapoishiwa na visodo wanavyopewa na mashirika. Sio wazazi wote wanaoweza kununua visodo, kwa hivyo "ni wazi kuwa huacha masomo wakati wa kipindi cha hedhi," Walea alisema.
Boroli iliandikisha wasichana zaidi ya 497 mwanzoni mwa 2019, Walea anasema idadi imeshuka katika kipindi cha pili. Karibu nusu ya wasichana hukosa madarasa kila siku, wale ambao hukosa wako katika madarasa ya juu. "Tunashuku kwamba hukosa kuhudhuria kwa sababu ya hedhi zao," Walea alisema.
AFRIpads, kampuni ambayo hutengeneza visodo vinavyoweza kutumika tena, imetoa msaada wa 200 [pakiti] ya visodo kwa FARM STEW kusambaza katika shule ya msingi ya Boroli katika kampeni iliyopewa mada ya "hedhi zangu, sauti yangu".