Kisa cha Phionah
Mimi ni Phionah Bogere mwanamke mwenye furaha wa umri wa miaka 23.

Nilimpoteza mama yangu nilipokuwa na umri wa miezi kumi tu. Baba yangu alifariki nilipokuwa na miaka sita. Kama yatima, nilianza kuishi na dada yangu mkubwa. Nilikuwa nikiamka asubuhi na mapema kwenda kuchota maji katika ziwa la Kyoga ambako kulikuwa mbali sana.
Maisha yalikuwa magumu. Dada yangu alikuwa na familia yake mwenyewe ya kuitunza kwa hivyo nilipelekwa katika kituo cha watoto yatima. Kwa namna fulani, kwa njia ya kujitahidi , Mungu aliniruhusu kupata mafunzo kupitia shule ya ufundi.
Kisha mwaka wa 2015, nilihudhuria mojawapo ya mafunzo ambayo Joy Kauffman alifundisha katika kanisa langu.
Wakati wa mafunzo, nilikuwa na hamu sana ya kujifunza na nilimuuliza maswali mengi. Wakati ulipoisha, nilimuuliza kama ningeweza kuwa mmoja wa timu yake. Baadaye, nilijifunza kwamba Mungu alikuwa amemwonyesha kuwa anapaswa kuanza timu ya FARM STEW lakini bado hakuwa amemwambia yeyote. Swali langu lilikuwa ni uthibitisho tu wa Roho Mtakatifu ambaye alihitaji kufuata usadikikaji wake. Nilikuwa na furaha sana na kushangaa kupata habari kwamba nilikuwa nimechaguliwa kuwa kwenye timu ya awali ya FARM STEW. Tangu wakati huo nimejifunza mengi.
Mimi binafsi nimefanya mafunzo 243 katika vijiji, shule, hospitali na makanisa na kuwafunza watu 16,694. Tuna karatasi za kuonyesha mahudhurio ya darasa la kila siku ili kuthibitisha hilo! Ninapenda kutoa mafunzo kwa wanakijiji jinsi ya kukuza na kutengeneza vyakula vipya, vya afya na kuwaelimisha vijana wadogo wa kiume jinsi usafi ulivyo muhimu katika kutunza miili yao.
Hata nami nina bustani la chombo katika nyumba yangu.

Hiyo hunisaidia kuhifadhi mshahara wangu, kuniruhusu kulipa karo za shule kwa ajili ya mayatima.
Kupitia kwa mafunzo, nimejifunza kujieleza na kupata ujasiri. Pia nimeweza kuhubiri ujumbe wa Mungu kupitia FARM STEW kwa sababu tunatumia Biblia kama msingi wa mafundisho yetu.
Ninawashukuru wafadhili wa FARM STEW!
Kwa sababu yenu, washiriki wengi wameboresha afya na tabia za kula na sasa wanafanya kilimo. Ninakutana na watu wengi ambao maisha yao yamebadilishwa kwa kutekeleza kile tunachofunza. Natamani ungekutana nao!
FARM STEW iishi maisha marefu! Phionah
Hapa kuna zaidi ya kisa cha Phionah ! Hapa kuna ushuhuda wa dakika 2 wa Phionah! Hapa kuna ushuhuda wa dakika 2 wa Phionah!