Visodo: Uhuru kutokana na Aibu
Tuna wasichana 534 zaidi ili kufikia lengo letu la mwaka 2019! $ 15 itatoa:
- Visodo 4 vya nguo vya kuosha katika kifuko cha deluxe cha usafi wa hedhi kilichotengenezwa na AFRIpads.
- Chupi 2 (tulijifunza wasichana hawana)
-Wakufunzi wetu wa FARMSTEW wanashirikiana na walimu wa shule kuelimisha na kuwapa vifaa wasichana hao kuvitumia
Jibu limekuwa ajabu!
Hivi ndivyo Naki alivyosema :
"Nina umri wa miaka 14 na nilianza kupata hedhi zangu mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na kukosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vile vichache vilivyoko ni bei ghali sana kuvinunua. Hivi visodo vipya vitaenda kunikinga wakati wa hedhi na kwa vile vinaweza kutumika tena, sina wasiwasi tena wakati nitakapokuwa nikipata hedhi. "

Unaweza kuondoa hofu kupitia usafi wa Mazingira
Katika mwaka wa 2017 tuliwahudumia wasichana 1,000!
Katika mwaka wa 2018, tulifikia watu 2,100!
Lengo letu la mwaka 2019 ni uhuru kutokana na aibu kwa wasichana 3,000! Shukrani kwa ukarimu wako, tunakaribia huko! Wasichana 535 zaidi!
Utakuwa ukiwasaidia wasichana kama Rebecca ambaye anataka kuwa katika shule zaidi kiasi kwamba ilimlazimu kuiba karatasi shashi (tissue paper)!!