Ilichapishwa
Oktoba 25, 2019

Mafunzo: Shukrani za Norah

Betty Mwesigwa

 Katika video,rangi angavu ya kitambaa cha shati la Norah inaonekana kuzungumza  furaha anayohisi  wakati anapozungumzia  kisa chake cha mabadiliko.

Norah ni mmoja wa  Kikundi cha Wanawake wa FARM STEW katika Kilima cha Wanyange Mashariki mwa Uganda!

Kila wiki ya kumi na tano wanawake katika nguo zao  za rangi angavu hukusanyika pamoja chini ya kivuli cha mti wa mwembe kwa aili ya upishi. Katika kijiji hiki cha mashambani huko Mashariki mwa Uganda, hakuna umeme wala maji ya mfereji hata hivyo wanawake hawa wana kitu kingine ambacho wengine hawana : furaha!

Sherehe hii  ni ya nini?        

Ni siku ya mafunzo ya FARM STEW. Mada ya siku ni chakula cha rangi za upinde wa mvua na kutengeneza mayai ya kuvuruga ya soya (tofu). Chakula cha "kando" cha ajabu ni kwamba jamii na hata mahusiano ya ndoa wanapata afya pia!

 Kikundi cha wanawake cha FARM STEW cha kilima cha Wanyange hukutana chini ya mwembe na Irene (akiwa kwenye nguo za kijani) akiwaongoza.

Hiyo ni kwa sababu dhamira ya FARM STEW ni kukuza afya na ustawi wa familia maskini na watu walio katika mazingira magumu duniani kote. Maono yetu yameongozwa na matamanio ya Yesu kwamba wote "wawe na uzima na kuwa nao tele" (Yohana 10:10). Kupitia mafunzo ya FARM STEW, washiriki hujifunza kushughulikia sababu za msingi za njaa, magonjwa, na umaskini, ikiwa ni pamoja na umaskini wa kiroho na mambo yanayohusiana na umaskini.

 Kabla ya FARM STEW, Norah alikuwa akihangaika kuwalisha watoto wake wanne na kulikuwa na wasiwasi na mume wake. Lakini mengi yamebadilika.  

Anasema,    

           "Ninatoa shukrani zangu kwa Mungu, ambaye alitupa maisha. Mungu amewawezesha nyinyi, watu wa FARM STEW ambao wameleta ujumbe huu kwetu FARM STEW inapowafundisha, inasaidia familia yako, jamii yako, na hata majirani zako. Hata waume wetu wanashangaa kuuliza, 'mlijifunzia wapi mambo haya?' Daima sisi huwaambia, ' 'FARM STEW, FARMSTEW!'

Masomo ya FARM STEW si kitu cha kuficha unafikia nyumba ya mtu, na unaweza kuona walifundishwa masomo ya FARM STEW. Katika nyumba zetu, sahani zinazungumzia FARM STEW. Katika nyumba zetu, wimbo ni FARM STEW "      

 Wimbo katika jamii hizi pia hutoa utukufu, heshima, na kumsifu Mungu kwa kile alichowatendea. Tumaini ni kwamba "mataifa yote yatakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha funuliwa"(Ufunuo 15:4).

Wanawake wote huonyesha shukrani zao kubwa kwa Betty na Jonah, wakufunzi wawili ambao kila Jumanne kwa miezi mitano iliyopita, wameleta "kichocheo cha  maisha tele".

Norah na wanawake katika kilima cha Wanyange  bado hawana kitu kimoja! Maji!

Tafadhali jifunze zaidi: https://www.farmstew.org/post/Water

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Betty Mwesigwa
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.