Kutana na Perusi, ambaye anapenda kula karoti kutoka shamba lake dogo!
Yesu anatamani sisi sote tuishi maisha tele (Yohana 10:10) na kushiriki maisha hayo na wengine. Nchini Uganda, zaidi ya thuluthi moja ya watoto chini ya miaka mitano wana hali ya utapiamlo sana. Upungufu hasa wa vitamini A na madini ya chuma umedhoofisha afya zao.
Kutana na mwanamke wa miaka 28 aitwaye Perusi, mama wa wavulana 3 na wasichana 2. Yeye ni mkulima na alikuwa akikuza soya kwa muda mrefu lakini kama karibu ya waganda wengine wengi hakuwapa watoto wake. Baada ya darasa la upishi yeye hutengeneza maziwa ya soya na bidhaa nyingine rahisi kwa ajili ya watoto wake. Anasema, "Mimi nalisha familia yangu na wanaonekana kuwa na afya zaidi kuliko kabla ya kupata mafunzo." Pia alikuwa mmoja wa familia 54 ambazo FARM STEW iliwasaidia kuanza bustani mwaka huu. Anaendelea kusema, "sasa nina bustani ya mboga nzuri ambayo ilikuwa ni matokeo ya FARM STEW kunipa miche ya mboga na kunihamasisha jinsi ya kuitunza vyema. Ningeweza kuchukua miaka miwili bila kula karoti lakini sasa ziko katika bustani yangu na ninakula kila wakati ninapotaka".
Je, ni kwa nini nijali kula karoti? Rangi ya machungwa katika karoti huwakilisha uwepo wa vitamini A. Vitamini A ndiyo inayoongeza kinga, inahifadhi nguvu ya macho na hatimaye inaweza kuokoa maisha.* Uwezo wa familia kukuza vitamini A wenyewe ni chanzo cha kichocheo kwa ajili ya maisha tele.
Karoti zinaweza kuokoa maisha kwa hakika. Kwa msaada wako tunaweza kubadilisha hali ya baadaye kwa Perusi na familia yake!