Kutana na Bakar, mkulima wa kujikimu aliyegeuka wakujitolea na mhamasishaji wa FARM STEW.
Bakar ni mkulima mdogo anayeishi katika kijiji cha Naluko, wilaya ya Iganga. Alihudhuria madarasa mawili ya lishe na upishi yaliyoandaliwa na FARM STEW Uganda. Anashuhudia kwamba tangu wakati mafunzo yafanyike katika kijiji chake, hanunui tena dawa kwa ajili ya homa na kikohozi. Bakar anasimulia jinsi mapacha wake walivyokuwa wakisumbuliwa na mafua mara kwa mara na sasa kile anachofanya ni kuchanganya kitunguu saumu, limau na asali ili kuzuia maradhi.
Bakar alihamasisha wakulima wenzake wadogo kushiriki katika mafunzo ya FARM STEW. Wenzake walimwomba awaalike wakati wowote fursa ya mafunzo itakapotokea. Bakar anamiliki bustani ya jikoni ambayo aliitengeneza kupitia kwa msaada wa mke wake baada ya mafunzo.
Yeye hujivunia jinsi bustani yake ya jikoni inavyoweza kutoa zaidi ya mboga za kutosha kwa ajili ya familia yake na uwezo wake wa kutekeleza mahitaji kwa watoto wake na mke bila kutumia fedha nyingi. Bakar asifia mafanikio yake kwa FARM STEW katika jitihada zake za kuboresha afya na ustawi wa familia za mashambani duniani kote.
Bakar atoa wito kwa watu binafsi ambao walikosa fursa ya kushiriki katika mafunzo kushauriana naye na wakulima wengine waliopata ujuzi mbalimbali katika lishe, kilimo endelevu na usafi wa mazingira.
Bakar na mkewe Namusbya Saluwha wanastawi kupitia kilimo cha kujikimu. Kwa kuuza baadhi ya mazao ya shamba na mboga kutoka katika bustani yao ya jikoni, wameweza kuendeleza familia zao.

Utakutana na Saluwha katika hatua ifuatayo!!