Upendo kwa mtazamo wa kwanza !
Unaweza kuwa umepitia changamoto ya kulisha watoto wako au wajukuu chakula kipya cha afya. Wakati mwingine wanakipenda na wakati mwingine wanalazimishwa. Hivyo ndivyo ilivyo nyumbani kwangu.
Katika sehemu za mashambani katika vijiji vya maskini vya Afrika ambako FARM STEW hufanyia kazi ni tofauti kabisa. Watoto wamechangamkia madarasa ya upishi wetu ya kiutendaji hata huwa na umati wao wakati chakula kinapokuwa tayari kupakuliwa. Wakufunzi wa FARM STEW huwa na furaha katika kuwasaidia watoto na huhudumu kama mfano kwa wazazi wao.

Inanikumbusha kuhusu Yesu anapoalika watoto wadogo kuja kwake. Wanakuja na sijawahi kuona hata mmoja akikataa vyakula vya FARM STEW.
Watoto hapo juu kutoka Mashariki ya Uganda wanaonja "mayai ya soya yaliyovurugwa" na "sufuria yenye rangi za upinde" (mboga mchanganyiko na soya) kwa mara ya kwanza.
Vyakula hivi vya protini ya hali ya juu na mboga zitawasaidia kukua halafu kama familia zao zinaelimishwa, wanaweza kuwasaidia wazazi wao kukuza vyakula hivi. Ni njia bora za familia kufanya kazi pamoja. Unaposhiriki daima huwa ni upendo wa kwanza!