Kahn katika Zimbabwe na FARM STEW
Kutana na Kahn, mwanagenzi wa FARM STEW na watoto nchini Zimbabwe katika nyumba ya mayatima ya Newstart!
Nchini Zimbabwe, FARM STEW ya kimataifa ina furaha kushirikiana na Kuda Vana!
Kuda Vana (ambayo ina maana ya "Kupenda watoto" katika lugha ya Shona) ni nyumba ya mayatima ambayo inafanya kazi ya kuwawezesha watoto walio katika mazingira magumu ya Zimbabwe si tu kwa kuishi lakini kustawi.
Susan Cherne, mwenyekiti wa Bodi ya Kimataifa ya FARM STEW aliwasiliana na Kuda Vana wakati alipokuwa akihudhuria kongamano la ASI la Kimataifa la mwaka wa 2019 huko Louisville, Kentucky kutafuta njia ambazo mashirika haya mawili yanaweza kushirikiana. Kuda Vana alijifunza kwamba FARM STEW ilikuwa ikifanya kazi ya kuboresha afya na ustawi wa familia maskini na watu walio katika mazingira magumu kwa kushiriki kichocheo cha maisha tele kote ulimwenguni.Ushirikiano wa asili ulianza na ndoto za kijana mmoja kwa ajili ya siku za usoni yenye kujitoshelezazenye yalichochewa.
Kuda Vana si nyumba yako ya mayatima wa kawaida. Wafanyakazi wao hutoa utunzaji wa kimsingi kwa kila yatima au mtoto aliyetelekezwa na kuletwa kwao na huduma za jamii. Watoto wanalelewa katika mazingira ya kinyumbani ya kikundi na kupewa upendo, lishe, usalama, huduma za afya, elimu, ujuzi wa maisha, mwongozo wa kiroho na kihisia ili kuwawezesha kuishi kwa kujitegemea zaidi, maisha yenye heshima na yaliyo bora. Wakati watoto wanapofikia umri wa miaka 18 katika utunzwaji, mpango wa mpito wa vijana wa Kuda Vana hutoa msaada wa mpito wa makaazi na karo kwa shule ya biashara au chuo kikuu.
Kila mtoto katika huduma ya Kuda Vana huchukuliwa kama wa familia na inapowezekana, kusaidiwa katika matumaini yao binafsi na ndoto zao. Hii ndio maaana Kuda Vana alikuwa na wasiwasi kuhusu mustakabali wa kijana Tendai mwenye umri wa miaka 16 ambaye amekuwa katika nyumba ya mayatima tangu alipokuwa mtoto. Tendai ana ulemavu wa kujifunza na kama kijana mdogo mara nyingi alionewa na walimu. Akiwa na umri wa miaka 15, hakuweza kusoma wala kuandika jina lake na alikata tamaa kabisa kufikia ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa kilimo au kujitegemea.
'
Kwa wakati na huduma kutoka kwa wafanyakazi huko Kuda Vana, Tendai hivi karibuni alijifunza kusoma. Yeye ni kijana wa ajabu ambaye ni mzuri katika kuimarisha mambo na kuchunga bustani huko Kuda Vana. Anaweza kufanya jambo lolote kukuza na huona fahari kubwa katika kazi yake. Hata hivyo, wafanyakazi walikuwa na wasiwasi juu ya kitakachotokea kwa Tendai wakati atakapofika miaka 18 na kuhitajika kuondoka kisheria katika Chuo cha Kuda Vana.
Dkt. Rick Westermeyer, Mkurugenzi wa wa kujitolea FARM STEW ya Zimbabwe, na mke wake alitembelea nyumba ya watoto wa Kuda Vana mwisshoni mwa mwaka. Walitembea katika bustani na kujifunza kuhusu maono ya Kuda Vana ya kuzindua mpango wa Mpango wa kilimo kustawi, mpango wa kuimarisha usalama wa chakula wa shirika na kukuza ujuzi wa maisha muhimu. Miezi michache tu baada ya mpango huu ilizinduliwa, Kuda Vana alikuwa na uwezo wa kuongeza ardhi yao ya kilimo na asilimia 500!
Dkt. Rick na mkewe pia walijifunza kuhusu Tendai na uhusiano wake na kilimo pamoja na mapambano yake katika shule ya jadi. FARM STEW ya Zimbabwe na African Orhan Care walijitolea kumpa Tendai udhamini kwa ajili ya kuhudhuria msingi wa mafunzo ya kilimo huko Harare pamoja na mfanyakazi wa FARM STEW wa kujitolea. Nafasi hii ilionekana kuwa kichocheo kamili cha Tendai kwa ajili ya kujiamini kwa matarajio yake ya baadaye kama mtaalamu wa kilimo.

Baada ya wiki mbili za kujifunza kuhusu kutengeneza mbolea, matandazo na kutengeneza mazao ya juu kutoka kwenye vipande vidogo vya ardhi, Tendai alipata cheti katika misingi ya kilimo. Kama mwanafunzi mdogo huko, anasema alihisi kukubaliwa na kujumuishwa na kila mtu hasa Khan Ellmers, mfanyakazi wa kujitolea wa FARM STEW alikuwa mvumilivu na mwenye manufaa katika kuhakikisha kwamba alielewa kila wazo. Tendai anasema kuhusu uzoefu wake:
"Ningependa kutoa shukrani zangu na kutoa shukrani kwa watu ambao walinifadhili kuwa na fursa ya kuhudhuria mafunzo haya ya kubadilisha maisha. Siku zote nimekuwa na ndoto za kupata nafasi ya kuwa na mafunzo hayo kwa kuimarisha ujuzi wangu kwani nina shauku kubwa katika kilimo. Sasa nina kitu ambacho naweza kufanya wakati umri wangu utanitoa nje ya Kuda Vana. Ningependa kuwa mkulima mkubwa wmenye uwezo wa kusambaza chakula kwa waduka makubwa ya mboga. Kwa sasa, ninatunza Ustawe wa mpango wa kilimo wa Kuda Vana, na si kubahatisha: Sasa nafanya mambo sahihi ninapo fanya kilimo. Hiki cheti kinamaanisha mengi kwangu. Hakuna anayeweza kuchukua maarifa niliyo nayo, nami nitachunguza ulimwengu. Kwa mara nyingine tena, asanteni sana kwa msaada. "
FARM STEW ina shukrani kwa ushirikiano wetu na Kuda Vana na ina tarajia kushirikiana katika njia zaidi ya kuhakikisha watoto walio katika hatari zaidi ya Zimbabwe si tu kwa kuishi bali kustawi.
Ikiwa ungependa kujifunza zaidi kuhusu kazi ya Kuda Vana na watoto yatima nchini Zimbabwe, tafadhali tembelea www.kudavana.org!
Ili kuona mahojiano kamili na Kahn Ellima bonyeza hapa!