Sherehe za FURAHA zinabubujika katika kilima cha Wanyange!!
Loh! Jinsi gani wiki hii inavyogeuka kuwa!!
Mradi wetu wa pili kwa sasa unaendelea huko Kilima cha Wanyange, Uganda!
Kijiji hiki kiliangaziwa katika blogi yetu ya hapo nyuma mwezi Oktoba (Unaweza kukumbuka Norah anayependeza akielezea kisa chake?)-na sisi tuna furaha ya kuujulisha ulimwengu kwamba hatimaye MAJI yamerudi eneo hili (baada ya miaka 2 ya kutembea kilo mita 5 kwa ajili ya maji kila siku)!
Tazama sherehe za furaha zinavyotiririka kutoka katika mioyo ya wanawake hawa!