Ilichapishwa
Novemba 26, 2017

Joy Nankwanga, "Siwezi kulalamika tena"

Joy Kauffman, MPH

Ni wakati wa kutoa shukrani tunapojiandaa kusherehekea zawadi bora zaidi iliyotolewa, Yesu.  Unapofikiria maisha yake, neno moja hujitokeza, huruma. Yesu alijawa na huruma zote kwa umati wa watu na watu binafsi. Vivyo hivyo tumeitwa kwa maisha ya huruma, hasa kwa wadogo kati ya hawa . Ninawashukuru kwa kujiunga na tukio hili la huruma liitwalo FARM STEW kwa matoleo yako ya ukarimu. 

"Siwezi kulalamika tena kwamba hakuna chakula cha kuwalisha watoto wangu."

Zawadi zenu kwa FARM STEW zitaziwezesha familia za mashambani kuhisi vyema! Watajifunza kula vyema, kukuza mazao mapya na kujitunza wenyewe. , Chukua kwa mfano,  Joy Nankwanga, katika kijiji cha Bubogo. Amekuwa na mafunzo mara mbili na FARM STEW na kuelezea matokeo yake na Robert. Joy alijifunza kukuza soya na kutengeneza maziwa kutokana soya. Anafaidika  kunywa maji zaidi. Alisema kuwa hakuwahi kunywa maji ya kutosha na matokeo yake alikuwa na matatizo ya utumbo. Sasa  anajihisi vizuri zaidi.  Pia alijifunza kutayarisha mchuzi wa tunda la fenesi  kutoka kwa matunda ya kijani ambayo hayajakomaa. Ni chakula chenye virutubisho ambacho ni cha kawaida katika Asia lakini hakijulikani barani Afrika.  Kwa ujasiri, Joy anasema, "kiwanja changu kina miti mingi ya matunda ya mafenesi na mimea,  siwezi tena kulalamika kwamba hakuna chakula cha kuwalisha watoto wangu."

Phionah huwafunza wanawake wenyeji kutayarisha matunda ya fenesi la kijani.

Alipoulizwa kuelezea uzoefu wake mpya wa maisha baada ya madarasa ya FARM STEW, alisema "Nilijifunza kwamba nyumbani kunahitajika kuwa na bustani ya jikoni. Pia nilijifunza kwamba chakula cha nyumbani kinahitaji kutayarishwa kutokana na aina ya mimea yenye virutubishi. Mbali na hilo, tunapaswa kuendeleza bustani za jikoni ili kupunguza matumizi ya chakula yasiyo ya lazima."

Joy anasema kwamba "kutoka herufi nane ambazo ni kifupi cha neno FARM STEW,  nimefaidika zaidi kutokana na herufi M. Nilijifunza kwamba tunapokula vizuri , tunajilinda dhidi ya magonjwa ya lishe. "

Wakati Joy Alipoulizwa kama FARM STEW ilichangia baadhi ya miche alisema, "katika mafunzo ya awali, FARM STEW imechangia mchicha, malenge, pilipili hoho na mbegu za biringanya. Alipanda mbegu hizi katika bustani yake ya jikoni. Alithibitisha kwamba katika mafunzo yaliyofuata FARM STEW  ilichangia miche kwa watu. "

Joy hukuza maharagwe ya soya kwa ajili ya chakula nyumbani kwake. Pia ana shimo la mbolea ambapo hutupa taka ya kikaboni.

Joy aliishukuru FARM STEW ya kimataifa kwa kuwafikia watu kwa mafunzo yanayolenga kuboresha maisha yao. Aliishukuru timu ya kuhamasisha jamii katika shughuli mbalimbali za afya ambazo ni pamoja na lishe, kilimo na usafi wa mazingira. Pia aliwaomba timu hiyo kuendelea na kampeni hiyo ili kukuza maendeleo.

 Ni kwa  jinsi gani ungeweza kuhamasisha Wakristo wa Uganda kuleta upendo wa Yesu kwenye vijiji na kuwezesha akina mama kuwalisha watoto wao? Unawasaidia akina baba kujifunza kufanya kazi kwa bidii katika mashamba na kuvuna mavuno mengi. Hata wanaume na wanawake wanajifunza kuheshimiana.

Tafadhali zingatia FARM STEW kwa utoaji siku ya Jumanne!

https://www.farmstew.org/donate

Mama huyu mchanga alikuwa akionja matunda ya fenesi yaliyo na rangi ya kijani   kwa mara ya kwanza! Ukarimu wako utaturuhusu kuwafikia wengi kama yeye katika  mwaka wa 2018. 

Ubarikiwe kwa ajili ya zawadi yako!

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Joy Kauffman, MPH
Joy ni mwanzilishi mwenye shauku wa FARM STEW.
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.