Ubunifu wa Umwagiliaji maji wa Jonah
Tazama uvumbuzi wa umwagiliaji wa Yona kwa vitendo!
Jonah Woira ni mmoja wa wakufunzi wetu bora nchini Uganda. Yeye ana shauku ya kukuza vyakula vya kienyeji, chakula endelevu na kwa ajili ya watu wanaoendelea! Yeye ni mjuzi sana kwa mambo ya kilimo (mtaalam katika sayansi ya usimamizi wa udongo na uzalishaji wa mazao) na tumefurahi kuwa naye kama kiongozi wa maswala ya kilimo wa FARM STEW ya Uganda tangu Oktoba ya 2019.
Mojawapo ya njia ambazo Jonah ameonyesha ujuzi wake ni katika uvumbuzi na ubunifu wake. Katika kijiji cha Kalungami katika wilaya ya Jinja Mashariki mwa Uganda hakuna pampu ya maji. Ile waliokuwa nayo ilivunjika miaka miwili iliyopita. Kwa sababu hakuna mtu aliyewahi kufunzwa jinsi ya kudumisha au kurekebisha pampu wakati kumetokea tatizo. Watu wa kijiji hiki sasa wanalazimika kutembea maili 2 (kama kilomita tano hivi) kupata maji kila siku.
Hata hivyo, hii haijasimamisha wanachama wa shule ya nyanjani ya Jonah ya FARM STEW kutokana na kutia bidii katika kumwagilia miche yao ya mboga. Suluhisho la ubunifu wa Jonah lilikuwa kuwafunza mbinu za unyunyiziaji mdogo wa maji kwa kutumia chupa za plastiki zilizotupwa kwa kuziweka juu chini! Hii huokoa safari za kwenda kuchota na husaidia kuifanya miche yao kuwa na maji na afya.
Je, yote haya ni rahisi? Kwa hakika sivyo. Je, mwishowe kuna thamani yoyote? Wale wanaofanya kazi na Jonah wanatoa hakikisho la ndio! Wamechangamshwa na mimea pamoja na mazao yao! Sio tu kwamba wanaweza kulisha familia zao wenyewe bali wanaweza pia kupata fedha kupitia kuuza mazao ya ziada kwa jamii ya eneo hilo.
Moja ya vipaumbele 5 vya FARM STEW kwa mwaka wa 2020 ni kurekebisha pampu ya maji katika kijiji cha Kalungami pamoja na kutengeneza visima 19 vingine na kuchimba visima 30 vipya. Ingawa lengo hili litagharimu $150,000, hili litatusaidia kubariki zaidi ya watu 15,000i! Hatuwezi kusubiri kuona njia za ajabu ambazo Mungu atazitumia kutusaidia kufikia lengo hili!!!
Jonah ameleta na anaendelea kuleta tofauti kubwa katika maisha ya wale anaowafundisha.Tunashukuru sana kwamba yeye ni sehemu ya wafanyakazi waFARM STEW!
"Imekuwa ni hali ya kusisimua ingawa ya changamoto ya uzoefu wa mafunzo kwangu. Imefungua akili na moyo wangu kwa uwezo ambao watu wanao na kwa utayari wao wa kujifunza, kufanya mazoezi na kusaidia jamii zao. Wenyeji wengi sasa wanatumia ujuzi mpya wa kilimo. Wengi wa watu hawa walikuwa hawajawahi kutaka kusikia kuhusu injili, hata hivyo sasa wanaulizia masomo ya Biblia! Wanaona kwamba tuna furaha sana kufundisha kila mtu na kutoa wakati wetu na rasilimali, inawasisimua. Mtazamo wetu wa unyenyekevu na utayari wa kusaidia si jambo la kawaida unaloweza kuliona hapa,"Yona Woira alisema.

Je, unapenda jinsi mbinu kamili yaFARM STEW ya kuendeleza watu inashughulikia sababu za msingi za njaa, magonjwa, na umaskini? Bofya kitufe cha zambarau nzuri upande wa kulia wa ukurasa ili kusaidia kuweka miradi kama vile ya Yona kwa nguvu!