Ilichapishwa
10 Oktoba, 2017

Jiunge nasi kusherehekea miaka miwili ya FARM STEW 

Joy Kauffman, MPH

 Miaka miwili iliyopita, wiki kama hii  niliwasili kama mtaalamu wa lishe wa kujitolea wa USAID nchini Uganda kwa mara ya kwanza.

Nilikuwa na maswali mengi sana akilini mwangu.  

Je, tungeweza kweli kutengeneza maziwa ya soya  ya maharagwe moja kwa moja kutoka kwenye mashamba ya wakulima bila ya umeme? Kama ni hivyo, je wanakijiji wangependa hilo? Na hayo makapi yaliyobaki kwenye kichungi tungeyafanyaje baada ya kukamua maziwa kwa vile hawakuwa na tanuru ya kuiokea ndani? Na tungeweza kubadilishaje ukweli kwamba hawakuwa wakiwapa soya watoto wao mara kwa mara? 

Nilianza FARM STEW na ujumbe rahisi, thamini mbegu zako, ziloweke na kuzichemsha! Zichanganye na safu ya upinde wa mboga! Utakuwa na faida zaidi kutokana na lishe ndani na watoto wako watazipenda! 

Kwa mshangao wanawake walishtuka kugundua kwamba kupitia soya waliyokuwa wakiipanda kwa miongo wangeweza kutengeneza maziwa na bidhaa nyingine nyingi za thamani. Nilishangazwa na uwezo mwingi uliopo  katika nchi ambayo asilimia 35 ya watoto wana utapiamlo. 

Tunaakisi miaka miwili iliyopita na kupanga kwa ajili ya maisha yetu ya baadaye. Jiunge nasi kusikia visa vya athari, jifunze vichocheo vichache na kuuliza maswali yako kuhusu FARM STEW!

Jiunge nasi kwa simu ya video katika: (viungo vitafanya kazi tu kwa wakati mwafaka)

Jumapili 10/15 saa kumi na moja jioni Saa za Kati (CT) kwa kubonyeza hapa au Jumatatu 10/16 saa tano asubuhi Masaa ya Kati (CT) kwa kubonyeza hapa.

Nitumieni barua pepe yenye anwani ya Joy@farmstew.org kama unataka taarifa zaidi kuhusu simu ya video!

Natumaini kukuona wakati huo!

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Joy Kauffman, MPH
Joy ni mwanzilishi mwenye shauku wa FARM STEW.
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.