Ilichapishwa
Juni 27, 2019

Huko Sudani ya Kusini,  uliokoa mtoto  anayeitwa Ketty na unaonekana kama  "Mwokozi"!

Joy Kauffman, MPH

Nilipowasili salama, niliingia katika wimbi la joto lenye makali zaidi ambalo sijawahi kuhisi.  Nikizungukwa na ndege kubwa zilizo wekwa alama kuwa ni mali ya Umoja wa Mataifa (UN) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP), vikumbusho kwamba Sudani ya Kusini ni taifa lenye vita ambapo kikosi cha 16,000 cha UN kinadumisha amani na asilimia 60 ya idadi ya watu wana hitaji kubwa la chakula. Nilipita mtihani wa uchunguzi wa Ebola (YIKES!), maafisa wa forodha walikagua visa yangu, na nikapata mzigo wangu juu ya moja ya kanda za mizigo yenye kutoa sauti kwa sababu ya ubovu kwenye kiwanja cha ndege.

"Momma Doreen" alitokezea na ghafla, nilikuwa "nyumbani" nikiwa na familia ya FARM STEW tena!

Joy na Momma Doreen, dada katika Kristo na huduma ya FAMR STEW 

Kwa nini niko hapa? Kwa sababu mulitoa ili tuweze kupanua FARM STEW kwa taifa hili lenye shida.  Kupitia matokeo yake, mapema mwaka huu Doreen Arkangelo, ambaye alikuwa kiongozi wetu wa timu katika kambi za wakimbizi, alihamia tena Sudan Kusini (baada ya kukimbia kama mkimbizi miaka kadhaa iliyopita). Pamoja na wakufunzi wanne wa kikristo wa FARM STEW, alianza kazi mara moja.  

Walifanya utafiti wa msingiwa kaya 500 katika vijiji 10 vya mashambani katika Jimbo la Magwi, katika wilaya ya ikweta ya Mashariki. Matokeo ya utafiti yalikuwa ya kushtua, asilimia 92 ya akina mama walikuwa na mtoto akiwa na homa na kuharisha katika mwezi uliopita na asilimia 64 yao watoto hao walifarikikatika kipindi cha miaka mitano iliyopita.  

Kwa pamoja, tunaweza kubadilisha idadi hii ya kutisha kupitia timu zetu nchini Sudan Kusini na katika maeneo mengine yenye usawa  katika hali ya kukata tamaa

Unaweza kushangaa, "ni kwajinsi gani zawadi yangu inaweza kuleta utofauti?"

Mtoto Ketty ni mfano mmoja wa maisha ambayo zawadi yako imeokoa.

Mnamo mwezi Februari nilipokuwa nafundisha wafanyakazi tisa wapya wa FARM STEW,  Ceasar, muuguzi na mkufunzi mpya wa Sudani Kusini alinionyesha picha ya mtoto Ketty.  Sikuweza kuileta kabla ili kuwaonyesha; ilikuwa inavunja moyo!  

Mtoto Ketty katika Februari 2019 akiwa na utapiamlo mbaya.

Ketty Achiro, mwenye umri wa mwaka 1, alibebwa na mama yake akionyesha upande wake wa nyuma. Sehemu zake za chini, ngozi yake imekunjana  kama mapindo ya pazia.kwa kweli sikujua kama angeweza kuendelea kuishi. Nilimhimiza Ceasar kuwaleta kwenye kituo cha afya, pamoja na kumakinikia kwa karibu na kuwafunza familia zaidi katika njia za FARM STEW, hasa sehemu ya "chakula".  Niliomba na kutumaini pia.

Nilipoona Ceasar mwezi uliopita, swali langu la kwanza lilikuwa, "Ketty anaendeleaje?"

 Yeye na Momma Doreen walitabasamu walipokuwa wakielezea jinsi mama wa mtoto huyu alikuwa AMECHUKUA mafunzo ya FARM STEWmoyoni.  Mamake Ketty alikuwa ameenda nyumbani na kumwambia mume wake kwamba mafunzo hayo yalikuwa ni "muhimu sana kuliko mafunzo yote ambayo amepokea kwa sababu ilikuwa msingi wa Biblia."  

Kwa pamoja, wazazi wa Ketty waliamua kutenda kile walichojifunza na kuokoa mtoto wao!Kwa sababu hiyo, Ketty ameongeza uzito mwingi, anafanya vyema, na wazazi wake wana shukrani sana! Ukarimu wenu ulifanya iwezekane kwa Ketty na watoto wengi kama yeye, kuokolewa!

Wadi ya utapiamlo ya Hospitali ya Wilaya ya Magwi hata waligundua!

La kusikitisha ni kwamba vituo vingi  vya "afya" vinaweza kutoa posho ndogo kwa wagonjwa kwa muda mfupi sana, lakini wazazi kwa uchungu wameachwa bila fahamu kuhusu jinsi ya kuzuia utapiamlo nyumbani.  

Benjamin, mkufunzi wa FARM STEW, akiwafunza wafanyakazi na akina mama ambao watoto wao wamelazwa katika wadi ya utapiamlo katika hospitali ya Kaunti ya Magwi

 FARM STEW inaweza kubadilisha hali hii ya huzuni! Kiongozi wa hospitali aliialika timu yetu kutoa mafunzo kwa wafanyakazi na wazazi.  Kwa msaada wako, kichocheo chetu cha maisha tele kinaweza kuwawezesha wazazi huko Sudan ya Kusini, Uganda na Zimbabwe ili kuokoa maisha ya watoto wao na kujifunza kuhusu Yesu!

Unaweza kuwa umeshangazwa kama mimi kusikia kwamba katika kijiji cha Ketty na vijiji vingine, watu sasa huita timu yetu ya FARM STEW "waokoaji!"  Nilipouliza "kwa nini?" walisema kwamba Kama Yesu,sisi huwafikia watu na kuwasaidia katika mahitaji yao kama alivyofanya.

Wenyeji wanaona tofauti kubwa kati ya mbinu za FARM STEW na mashirika mengine.

Kwanza, mashirika mengineyo mengi  huwa na wafanyakazi ambao wanabakia katika ofisi mjini wakisubiri watu waje kwao.  Wakufunzi wa FARM STEW hukutana nao katika nyumba zao ndogo na mashamba yao na hawatoi posho tu, lakini huwafundisha kukuza aina ya vyakula mbalimbali.

Pili, tunawashangaza watu kwa kuanzisha kila mafunzo katika kijiji na maneno ya Yesu yaliyoandikwa katika Yohana 10:10, "nimekujaili muwe na uzima na kuwa nao tele!" Mtazamo wetu wa kiroho ni wa kipekee kwani makundi mengi yanalenga tu juu ya mahitaji ya kimwili.

Hatimaye, tunafanya kazi na viongozi wa eneo hilo. FARM STEW ilishirikiana na  machifu 10 wa eneo  kusimamia viwanja 13 vya jamii ambapo wanakijiji walipanda paundi 880 ya  maharagwe ya soya  uliyotusadia kununua mnamo mwezi Machi.  Mavuno kutokana na viwanja hivi  yatazidi paundi 20, 000   na yatasambazwa kwa ajili ya upanzi kuanzia mwezi Agosti.  Wanakijiji ambao walisaidia kupanda viwanja vya jamii walipata paundi 3 za mbegu ya soya kila mmoja na kuwa na jumla ya paundi 1,400 na mbegu nyingine za mboga  kwa ajili ya viwanja vyao vya nyumbani.

Ben, mkufunzi wa FARM STEW anapanda soya na kundi la wanakijiji. Kamba husaidia kuhakikisha Safumlalo hupandwa sawa na nafasi mwafaka.

Kila kitu nchini Sudan Kusini ni beighali sana kwa sababu sekta nyingi za eneo hilo zimeharibiwa na bidhaa za nje zinazokuja na lebo ya bei ya hatari.  Katika miezi yetu 6 ya kwanza, tulihitaji kutumia zaidi ya $42,000 kwa kuajiri, kutoa mafunzo, kuandaa, na kuhamasisha timu yetu na kutoa vifaa vya kuzindua kazi katika vijiji 10.

Uwakili wenu mzuri wa ukarimu wenu ni lengo letu na linakua kote katika Kaunti ya Magwi, Sudan Kusini na Uganda na Zimbabwe ambako timu zetu zinakaa. Kwa baraka za Mungu na uwekezaji wenu wa kuendelea, familia nyingi zaidi zitabarikiwa.

Je, sisi ni "waokoaji"?  Hapana, lakini tunamjua Mwokozi. Wanakijiji wako sahihi; sisi tunakuja "kuokoa" na ujumbe wetu, kama Wake, ni "habari njema kwa maskini." Wanakijiji wanaupenda ujumbe huu!

Ili kujifunza zaidi kuhusu kile kinachotokea, unaweza kuja na kujionea mwenyewe kwa kujiunga nami  kwa simu ya video siku yaAlhamisi, Juni 27 na/au Jumapili, Juni 30 saa kumi na mbili jioni CT?  Ninaweza kutoa video na visa vya ziada ili kufanya barua hii kuwa na uhai!  Nitumie barua pepe katika joy@farmstew. orga kiungo! Siwezi kusubiri zaidi kukuonyesha ishara za maisha tele.

Lengo letu kuu katika Sudani Kusini nikusambaza ujumbe huu katika makanisa na jamii ili watu waweze kuishi kwa amani na ndege za Umoja wa Mataifa zilizojazwa vyakula na walinda amani hatimaye hazitahitajika.

Machifu wa Afrika na wafanyakazi wa hospitali  ya kaunti ya Magwi wote  wanauliza FARM STEW kufunza familia zaidi. Tunasikia kilio hiki cha "" Makedonia ","Njooni mtusaidie, "si tu katika Sudani Kusini lakini katika maeneo yetu yote na zaidi!   

Itachukua maombi, wakati na fedha kuitikia kilio!  

Je, utaendelea kuwa mdau muhimu kwenye timu ya  FARM STEW kwa kutuma zawadi ya ukarimu katika bahasha iliyoambatanishwa leo? Tunataka kuitika kilio, na tunahitaji msaada wako wa kuchanga $42,000 kufikia mwisho wa Julai kuendelea kusonga mbele. Zawadi yako ya $74 leo itasaidia kudhamini madarasa mawili ya kijiji.

Hapa ndipo kuna sababu kwa nini niko katika timu ya FARM STEW  na kwa nini nakualika kwa ujasiri uwe mshiriki muhimu!  Wakati wanawake walikwenda kaburini kutunza mwili wa Yesu, malaika waliwasalimu, wakisema, 'kwa nini mnamtafuta anayeishi kati ya wafu? " Wakishawishika na malaika kwamba Yesu alikuwa hai, wanawake waliondoka kaburini kueneza habari njema! Hata hivyo, kwa wanafunzi, maneno yao yalionekana kama "hadithi isiyo na maana."   Lakini Petro alikimbia kwenye kaburi, "akaona nguo za kitani zikiwa zimelala zenyewe na akaondoka, akishangaa mwenyewe kile kilichotokea," Luka 24:12.  

FARM STEW "inatafuta wanaoishi  miongoni mwa wafu." Kimiujiza, tunaona ufufuo ukitokea kila siku! Ninamsifu Mungu kwa ajili ya yote aliyotuwezesha kutimiza na ni maombi yangu ya   kwamba Roho Mtakatifu atakusaidia kutoa kwa ukarimu leo!

 Mbarikiwe sana . 

Betty, kiongozi wa FARM STEW Uganda, amechukua mayatima saba na kuwasaidia na shamba lake kubwa na msharaha wa FARM STEW.  Hukaa naye wakati mimi niko huko.  Ukarimu wako hufanya familia hii ya FARM STEW iwezekana!


Joy Kauffman, MPH

Mwanzilishi na Rais

FARM STEW ya Kimataifa 

PS: zawadi zenu za kifedha zinabadilishwa na FARM STEW katika elimu ya kuokoa maisha kwa wazazi, mshahara wa haki kwa wakufunzi wetu, pikipiki, mafuta, mbegu, visodo vya AFRI, na mengi zaidi; yote haya yamewekwa wakfu kwa ajili ya kuwezesha wanakijiji kustawi. Je, utapanda ukarimu, kutusaidia kukutana au kupita lengo letu la $42,000?  Zawadi yako ya $74 itadhamini madarasa mawili ya kijiji.

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Joy Kauffman, MPH
Joy ni mwanzilishi mwenye shauku wa FARM STEW.
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.

Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.