Kwa ulinzi wa Mungu na soya
Soya ilileta uhalisia wa kibinafsi kwangu. Kwa miaka nimekuwa nikiwaambia watu ukweli kwamba zaidi ya kikombe kimoja cha maziwa ya soya kila siku kinaweza kupunguza nafasi ya wanaume kupata ugonjwa wa saratani ya kibofu kwa asilimia sabini ( 70%). [1] Juma lililopita baba yangu, ambaye amefuata ushauri wangu wa afya lakini hajawahi penda soya, aligunduliwa kuwa na saratani ya kibofu iliyo kua kwa haraka. Hofu ya soya husababisha watu wengi, asilimia themanini na nane (88%) katika utafiti huo huo, kuikataa waziwazi.
Soya pia ni ya kibinafsi kwangu kwa sababu mimi hufanya kazi kwa niaba ya watapiamlo nchini Uganda ambapo soya ni chanzo pekee cha protini ya ubora wa juu kwa maskini. Hakuna chakula kingine cha mimea kilicho na amino asidi tisa muhimu zihitajikazo kwa lishe la binadamu. Ukosefu wa maarifa kuhusu thamani ya soya husababisha familia nyingi ambazo zinaikuza zisiwape watoto wao wenyewe ambao asilimia thelathini na tano (35%) huwa na utapiamlo uliokithiri.
Huwezi kusema neno "soya" siku hizi bila kuanza mdahalo. Wamarekani wengi wanashangaa kama soya ni kitu muhimu cha kuzingatiwa kwenye lishe kamili. Tunapaswa kujua vilivyo. Utafiti wa Kitaifa wa kijiografia ulitambua Loma Linda kama ukanda wa watu wenye kula vyakula vya mboga na matunda na wenye maisha marefu( Blue zones) Dan Buettner, Mtafiti wa mambo ya afya na maisha marefu aligundua kwamba Waadventista wa Sabato wanaoishi huko wamefanya soya kama mojawapo ya vyakula vyao bora [2]Urefu wa maisha (Longevity) wa wakazi wa ukanda huu (Blue zones) katika Okinawa nchini Japan ulikuwa ukihusishwa na soya pia. Buettner anasema kitendo rahisi cha kula maharagwe kinaweza kuongeza miaka 4 ya maisha. Hivyo kitu kidogo kuhusu maharagwe hayo ni cha muhimu sana.
Soya imethibitishwa kusaidia kuzuia aina nyingi za saratani[3]na hata ukosefu wa nguvu ya mifupa (osteoporosis)[4] lakini wengi wetu tunaacha maziwa ya soya na kuchagua njia nyingine zisizo za maziwa. Je, mtu yeyote amegundua kwamba hakuna gramu yoyote ya protini katika maziwa hayo mengine yote ikiwa ni pamoja na mlozi, kitani , nazi na korosho? Kwa wenye kula vyakula vya mimea na hasa ambao hawali hata vyakula vitokanavyo na wanyama (vegans), haipasi kususia protini ya ubora wa juu katika maziwa ya soya gramu 8 kwa kikombe.
Nitapeana kwa wakosoaji, nyingi ya soya inayotumiwa katika nchi hii ni ya kijenetiki na yenye kusindikwa sana. Wala hakuna yoyote ile inayofaa kwa mbegu hii ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu. Soya pia inakashifiwa kwa sababu ya kukosa kupambana na sababu za lishe kama asidi ya phytic ambayo huzuia ufyonzaji wa madini. Wakati nilimuuliza Mungu "kwa nini?" Naamini alifunua ukweli ambao sasa unafaidisha maelfu nchini Uganda. Natumai utanufaisha familia yako pia.
Wakati maharagwe ya soya na mbegu nyingine zinapokauka mapema kabla ya mavuno, virutubishi vyao huwa chini na hukosa kupatikana. Hii ni baraka kwa sababu, bila ukweli huo, mbegu hizo zitaharibika badala ya kuhifadhika majira ya baridi. Utaratibu wa kuishi wa maisha ya binadamu zaidi kanda ya kitropiki hauwezekani bila uwezo wa mbegu kufunga virutubisho vyake zaidi. Fikiria Yakobo alivyohifadhi mbegu nchini Misri kwa miaka saba!
Lakini kama vile mkulima apandavyo mbegu katika udongo wa majimaji unaotiwa joto na jua wakati wa mvua, sisi pia tunaweza kuongeza upatikanaji wa virutubisho kwa njia ya kulowesha na kuzitia joto mbegu. Wakati nafaka na kunde hufaidika kutokana na kuloweshwa, soya huhitaji masaa kumi hadi kumi na mawili (10-12) ya kuamsha ving'ang'anizi vinavyowezesha kupatikana kwa virutubishi. Utapata chakula bora kwa kuchemsha kwa dakika ishirini! Kutokana na maharagwe hayo unaweza kufanya maziwa yako mwenyewe, tofu, au kuendelea kuyachemsha na kuyala kama maharagwe mengine yoyote. Rangi ya manjano ya soya inatoa taswira ya kuwa sufuria ya dhahabu iliyojaa nyuzi, madini, na amino asidi. Hazina hii ni ya kipekee.
Hivyo furahia soya, kuna nguvu katika mdundo!
[1] Jacobsen B, Knutsen S, Fraser G "Je, kunywa kiwango kikubwa cha maziwa ya soya hupunguza matukio ya saratani ya kibofu cha mkojo? Utafiti wa afya Waadventista (Marekani)" Sababu za saratani na Udhibiti, 1998, 9, 553 -557. https://Link.springer.com/article/10.1023/A%3A1008819500080
[2] Dan Buettner, kanda za maisha marefu (Blue Zones); Sayansi ya kuishi kwa muda mrefu. Kijiografia ya Kitaifa, Washington DC, 2016. P 35 & 23.
[3] Messin,M, Messina,V. Detchell, K. Soya rahisi na afya yako, Avery Publishing Group, New York, 1994.
[4]Vichuda LousuebsakulMatthewsabSynnove F. KnutsenaW. LawrenceBeesonaGary E. frasera "maziwa ya soya na matumizi ya vyakula shajara huhusishwa kibinafsi na utulizaji wa mfupa wa kisigino kati ya wanawake waliokoma kupata hedhi: Utafiti wa afya ya Waadventista-2" utafiti wa lishe wa 31, toleo la 10, Oktoba 2011, kurasa 766-775 https://Doi.org/10.1016/j.nutres.2011.09.016