Ilichapishwa
Novemba 28, 2017

Mke wa Bakar Saluwah anahisi vizuri zaidi! Sababu? Anakunywa maji, kula maharage ya soya na anasema, "pamoja na mume wangu; Sisi... hukuza mboga zetu wenyewe."

Betty Mwesigwa

Mkufunzi wa FARM STEW Robert Lubega. Wao hukuza biringanya, nyanya, na mboga nyingine. Bakar na mkewe Saluwah sasa wanastawi kwa kilimo cha kujikimu. Kwa kuuza baadhi ya mazao ya shamba na mboga kutoka katika bustani yao ndogo ya jikoni, wameweza kuendeleza familia zao. 

Saluwah anasema, "Mimi sikujua kamwe kwamba tunaweza kupata maziwa kutokana na  soya. Mimi nilikuwa nikinunua na kutumia maziwa ya ng'ombe. Nilipojifunza kuhusu maziwa ya soya na jinsi ya kuyatayarisha kutokana na maharagwe, nilianza kuyaandaa kwa ajili ya watoto wangu. Nilitambua uboreshaji wa hatua kwa hatua katika afya yao."

Pili, anasema "Nilikuwa nikinywa maji kidogo. Wakati mwingine midomo yangu ingepasuka na kuanza kushangaa kama nilikuwa mgonjwa. Wakati mwingine nilifikiri kwamba labda mwili wangu una upungufu wa baadhi ya madini. Nilipojifunza kutoka FARM STEW  kwamba moja ya dalili za kutokuwa na maji mwilini ni kukauka kwa midomo, nilianza kunywa maji kila mara. Midomo yangu haipasuki tena, afya yangu imeimarika sana na sasa najihisi vizuri. "
Saluwah pia anasema "kabla ya FARM STEW kutufunza, nilikuwa nikinunua biringanya  na mboga nyingine kutoka kwa wachuuzi.  Kwa sasa hatununui tena kwa sababu mimi na   mume wangu tuna bustani ya jikoni na tunakuza mboga zetu wenyewe. "
Saluwah na mumewe Bakar waonyesha bustani ya jikoni kwa mkufunzi wa FARMSTEW, Robert Lubega. Wanakuza biringanya, nyanya na mboga nyingine.

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Betty Mwesigwa
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.