Ni kwa jinsi gani FARM STEW inafafanua chakula cha msingi wa mmea?
Profesa Hussein, (kutoka Idara ya Lishe ya Chuo Kikuu cha Afrika)
Mimi pia nathamini maoni yako. Ni muhimu kukumbuka kwamba watu hufafanua "lishe la mboga " tofauti. Hapa ipo nukuu kutoka Wikipedia.
Mlo wa mboga ni vyakula vinavyotokana na mimea, ikiwa ni pamoja na mboga, nafaka zisizokobolewa, njugu karanga, mbegu, kunde na matunda, lakini na bidhaa chache za wanyama au bila. [1][2] matumizi ya kifungu hicho cha maneno kimendelea kubadilika muda baada ya mwingine na mifano inaweza kupatikana kwa kifungu hicho cha maneno "lishe la mboga" hutumika kwa kumaanisha mlo usiokuwa na bidhaa za wanyama (yaani vegan) , ambayo haina chakula kutoka vyanzo vya wanyama, vya mboga ambayo ni pamoja na mayai na maziwa lakini hakuna nyama, na kwa mlo wenye kiasi cha bidhaa za wanyama, kama vile mlo wa nusu mboga na nusu bidhaa ya wanyama ambayo huwa na kiasi kidogo cha nyama. [1]
Wakati FARM STEW inapotumia neno, hatusemi kwamba chakula hadi kiwe hakina bidhaa za wanyama (vegan). Tunatumia toleo lililochukuliwa la piramidi ya vyakula vya uponyaji lililotengenezwa na Chuo Kikuu cha Michigan. Tunaikubali ili kuondoa vyakula vilivyoamuliwa kuwa najisi kwa Biblia na Koran kama maana sisi ni shirika lenye msingi ya imani na vyakula hivi vimethibitishwa kuwa vimenajisiwa sana katika hali nyingi. Mabadiliko hayo yanapokelewa vizuri sana katika jamii ambapo wakufunzi wa FARM STEW wamepelekwa, kwa sasa wakifundisha watu 47,000.
FARM STEW pia inalenga kuongeza vakula mbadala kwa sababu kile unachosema kuhusu asilimia kubwa ya vyakula vya wanga k huonekana kuwa hali ya kawaida miongoni mwa maskini wa dunia. Tunatumia UN-FAO ilitengeneza kiwango cha Chini cha Vyakula Tofautitofauti kwa wanawake kama njia ya kutathmini na chombo cha ufuatiliaji. Kwenye tovuti hiyo, kuna jibu la kuvutia sana kwa swali hilo "kwa vyakula tofautitofauti muhimu?" Inasomeka kuwa:
Vyakula mbalimbali na makundi ya chakula ni vyanzo vizuri vya virutubishi vinavyohitajika ukubwa na vile vinavyohitajika kwa udogo, hivyo mlo mbalimbali bora huhakikisha utoshelevu wa virutubishi. Kanuni ya tofauti za vyakula imeingiana katika ushahidi wa mfumo wa chakula cha afya, kama vile chakula cha Mediterranean na chakula cha "DASH" (mkabadala waChakula wa kusitisha shinikizo la damu. Na kuthibitishwa na miongozo ya misngi wa vyakula bora Shirika la Afya Duniani (WHO) labainisha kuwa chakula chenye afya kina matunda, mboga, kunde, njugu karanga na nafaka isiyokopolewa.
Mlo tofauti ni una uwezekano mkubwa wa kukutana na hali mbili tofauti, mahitaji ya afya ya wanadamu wanayojulikana na yasiyokulikana. Mbali na elimu yetu ya protini, asidi ya mafuta iliyoi muhimu, mahitaji ya vitamini na madini, maarifa mapya kuhusu madhara ya afya mbalimbali ya misombo ya bioactivu inaendelea kukua. Kuzingatia vyakula vya mimea peke yake, kwa sasa inakadiriwa kuwa kuna kiasi cha bioactivu zenye kemika za phyto 100,000 na kwamba "zinaangalia athari za afya zinazohusiana na mboga, matunda, beri, na matumizi ya nafaka isiyokobolewa inaweza kuelezewaa kwa hatua pamoja ya kemikali za phyto mbalimbali na virutubisho vingine" (Nordic mapendekezo ya lishe 2012. Copenhagen: Baraza la mawaziri Nordic).
Napenda makabiliano kwamba kama ilivyoelezwa hapo juu, chakula cha mboga kina faida nyingi kwa watu wote na kina elezewa sana katika vitabu.
Profesa Hussein, baraka kwako katika kazi yako ya kuongeza vyakula tofauti tofauti kwa watu wote, hasa maskini, kupitia kwa ya kazi yako!
Joy Kauffman, MPH
Rais na mwanzilishi wa FARM STEW
