Bustani: Uhuru kutokana na Njaa
Uganda inajulikana kama "Lulu ya Afrika!" Ukiangalia, uzuri katika nchi na watu wake unang'aa kila mahali. Lakini wakaazi wengi wa vijijini wanaonekana kuwa hawana uwezo wa kuvunja ganda ili kupata lulu.
Moja ya vikwazo muhimu zaidi ni mtazamo wao. Hawana matumaini na wanakukosa motisha.
"Kabla ya kuja , fedha kidogo amabzo mume wangu angeweza kupata kama mshonaji wa viatu hazikuwa zikitosha kulisha familia na kulipa karo ya shule kwa watoto wetu wanane. Mimi niliogopa kulima (kilimo) kwani nilifikiri ni laana, "alisema Fatuma (katikati hapa chini).
Zawadi zako husaidia kubadilisha akili na mioyo ya watu waliopewa mafunzo na FARM STEW.

Robert, mtaalamu wa kilimo wa FARM STEW, (kwa kijani), alitumia muda na David, na mkewe Fatuma hivi karibuni wakati wa moja ya ziara nyingi za nyumbani za FARMSTEW. Kwa kweli alivutiwa na bustani yao mpya inayostawi. David, Fatuma na familia zingine nyingi zilionyesha matokeo ya mbinu walizojifunza kutoka kwa FARM STEW. Hapa kuna vile Fatuma alivyoshiriki:
"Baada ya FARMSTEW kutufundisha faida ya bustani na kutupatia mbegu za mboga, ilifanya hatua yangu ya mageuzo. Sasa ninajiona kama mtu muhimu sana katika jamii yangu. Kwa kulima mboga, tunaweza kumudu kuwatayarisha kula na tuna afya bora zaidi.
Baadhi ya wananchi katika jamii sasa wanakuja kununua mboga za majani. Sasa nina mboga katika hatua zote za ukuaji;zilizo bado katika shamba la miche zilizokua na zile zilizo tayari kuvunwa. Kwa kuuza zile za ziada, sasa ninaweza kuwapeleka watoto wangu shule na kutimiza mahitaji ya msingi ya nyumbani. Ninamsaidia hata mume wangu."
Wanandoa hawa wenye furaha wananikumbusha ukweli rahisi: FARMSTEW ni kazi nzuri ya umisionari! Nukuu hii iliongoza kazi ya FARM STEW:
Wakati mbinu sahihi za kilimo zinatekelezwa, umasikini utapungua zaidi kuliko ulivyo sasa. Tuna nia ya kuwapa watu mafunzo ya uzoefu kuhusu kuboresha ardhi, na hivyo kusababisha ari kulima nchi yao ambayo haina kilimo kwa sasa. Kama tutakamilisha hili, tutakuwa tumefanya kazi nzuri ya utume. — Ellen G. White, barua 42, 1895
Fatuma hayuko peke yake, kutokana na mafunzo ya FARM STEW maelfu ya maisha ya watu na ardhi imebadilishwa.


Asanteni kwa kufanya kazi hii iwezekane ili wenyeji wa Afrika waweze kupata baraka katika udongo!