Ilichapishwa
Machi 18, 2019

Naomi hangeweza kuhudhuria shule kwa sababu ya hofu na aibu. Zawadi yako inaweza kubadilisha maisha kama yake!

Joy Kauffman, MPH

Wengi wa wasichana wa  kiafrika wanapoingia umri wa kubaleghe, mara nyingi huwa sababu kwao kuacha  shule. Aibu na hofu huwazuia kutohudhuria wakati wanapopata  hedhi kwa hivyo wanaachwa nyuma na kuacha shule kwa idadi kubwa.  Kutoka wakati huo, siku zao za usoni huingia giza.

Wasichana ambao wameacha shule mapema mara nyingi huwa akina mama wa mapema hali inayoendeleza mzunguko wa umaskini kwa watoto.

 

Je, unaweza kufikiria binti  au mjukuu wako anayekabiliwa na hali hiyo ya kutisha?

Kwa  zawadi zenu, FARM STEW inaweza kubadili maisha ya wasichana kama vile Yesu alipobadilisha hatima ya mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu ambaye alimfikia na kugusa pindo la vazi lake. Yesu alimwita "binti," na akamponya.  

Zawadi zenu zimewasaidia wasichana 3,100 kama Sara na Naomi (utakutana nao ukurasa unaofuata) katika njia sawa.  Ni sehemu ya usafi, herufi "S" katika FARM STEW ni kichocheo cha maisha tele.  

 Kuhakikisha kuwa tunasaidia kwa kweli, wiki iliyopita timu yetu ilisafiri kwa saa moja kupitia barabara za mchanga zilizotupeleka hadi  shule ya msingi ya Nawankwale.  Benon Waluube, Mwalimu mkuu, aliwasalimu kwa furaha na  kuishukuru FARM STEW (na wewe) kwa ajili ya kutoa visodo na mafunzo kwa wasichana 71 mwezi wa Aprili mwaka jana.  

Benon kwa furaha alituonyesha rekodi za usajili kwa miaka miwili kuonyesha kwamba usajili umeongezeka kutoka 70 hadi 85 katika  gredi ya 6 na kutoka 36 hadi 47 wasichana katika gredi ya 7.  Alisema kuwa kuongezeka kwa usajili na mahudhurio yalikuwa ni matokeo  ya moja kwa moja ya usambazaji wa visodo na mafunzo ambayo yaliwezeshwa na zawadi yako kwa FARM STEW.  Katika kichocheo chetu cha maisha tele herufi "S" inayosimamia Usafi (Sanitation) inafanya kazii!

Lakini hilo halikuwa zuri la kutosha!  Tulitaka kusikia kutoka kwa wasichana moja kwa moja! Je, maisha yao yamebadilika?

Betty Mwesigwa, mkufunzi wa kilimo wa FARM STEW Uganda na Tamara Schoch, mfanyakazi wa FARM STEW wa kujitolea alikutana na kundi la wasichana 25 walio baleghe na mkufunzi mmoja wa kike.  Kwa mara ya kwanza, wasichana waliona haya, lakini polepole walianza kujibu maswali yetu.  

 

Naomi alizungumza kwanzaakielezea kwamba katika siku za nyuma alitumia nguo za zamani ambazo zilisababisha "kuungua," (pengine kutokana na maambukizi ya njia ya mkojo ambayo asilimia 24 ya wasichana wa Uganda huathirika).  Angeweza kuwa makini jinsi alivyotembea kwa hofu ya kitambaa kusonga au kuanguka. Kisha Sarah alielezea kwamba kama kungekuwa na  na kuvuja tu, angekejeliwa mno, kwa hivyo alifanya uamuzi wa kimantiki wa kuacha kuhudhuria shule katika siku hizo.

 

Tuliwauliza wasichana wote  wanyoshe mikono yao kama walikaa nyumbani wakati wao wa hedhi kabla ya kupata visodo.  

Karibu kila mkono uliinuliwa.  Walikuwa hawajulikani walipo
kwa sababu tu walikuwa wanakua. Huzuni kubwa!

Kisha Naomi alielezea, kwa tabasamu kubwa kwamba visodo vipya alivyopewa na FARM STEW ni vizuri na havisababishi kuungua. Anaweza kuvaa kisodo kimoja na kuleta cha pili na anaweza kubadilisha kimoja baada ya kingine kulingana na hitaji. Wasichana walisema ni rahisi kuvifua na kuvikausha visodo kwa haraka.

Sasa Naomi, Sara na marafiki zao wanaweza hata kushiriki katika darasa la elimu ya mazoezi ya mwili (PE) bila hofu.    

Mwalimu hajui ni nani aliye katika hedhi zake. Mungu asifiwe, hivyo ndivyo inapaswa kuwa!  

 

Wasichana wanakuja shule, wako huru kutokana na aibu. Hii ni kutokana na huruma yako!  Kitendo hiki cha wema kiliwashawishi   kwamba wanapendwa na Mungu na watu kama wewe!

 

Maisha yao na ya elimu ni muhimu! Ni asilimia 25 tu ya wasichana wa Uganda na hata wachache zaidi katika nchi ya Sudani Kusini huhudhuria shule ya sekondari. Matokeo ni dhahiri, asilimia 62 tu ya Waganda na asilimia 16 ya wanawake wa Sudan Kusini wanaweza kusoma. Elimu ya juu inahusiana mkabala na kiwango cha chini cha asilimia thelathini (30%) ya kuwa na watoto wenye utapiamlo. [1]   ikiwa tunaweza kuwasaidia wasichana kupata elimu wanaweza kulisha na kubadilisha Mataifa.

 

Vipande vyote vyaingiliana pamoja katika  kichocheo cha maisha tele cha FARM STEW.  Je, utaendelea kuielezea?

 

Kutokana na ukarimu wako, tuliunda mpango ufuatao ili kupanua juhudi hii:

  1. Nunua vifaa 3,000 vya hedhi kiasi kikubwa  zenye visodo vitatu vikubwa, kisodo kimoja kikubwa zaidi na mfuko wa kiheshima wa kubebea.  Vyaweza kuoshwa na kudumu kwa mwaka mzima. Vyote hutendenezwa nchini Uganda na kuleta ajira kwa wanawake zaidi ya 200 walio  katika kazi nzuri.  Hii hujumlisha ahadi yetu ya usafi wa mazingira na biashara, viungo viwili muhimu katika kichocheo cha FARM STEW.
  2. Nunua jozi 6,000 za nguo za ndani kwa sababu tulijua kwamba wengi wa wasichana  hawana nguo za ndani!  Haiwezekani kutumia visodo bila nguo za ndani. Kundi hili la viziwi katika Kanisa la Jinja la Waadventista litatengeneza nguo hizi za ndani. Wakufunzi wetu wamekuwa wakiwasaidia kuendeleza mpango wao wa biashara ambao unajumuisha kutengeneza sare za shule na vitu vingine vya kuuza.
  3. Kuhamasisha wakufunzi wetu 22 wa FARM STEW wa Afrika kutoa elimu ya afya kwa msingi ya Biblia, visodo, na nguo za ndani kwa wasichana 3,000 wa vijijini, Afrika.  Hii ni sehemu muhimu sana kwa sababu tunabadilisha mitazamo na tabia ambayo inaweza kusababisha maisha tele.  
Mmoja wa wale viziwi katika kundi la kushona nchini Uganda wanatengeneza nguo za ndani!

Tunafurahi sana kukutana na mahitaji ya usafi ya wasichana  3000 wa kiafrika  vijijini  huku tukiunda fursa za biashara kwa mamia ya watu walio katika mazingira magumu! Utabarikiwa kwa kujua kwamba wewe ni sehemu ya kazi ya Mungu katika kufikia mmojawao wa hawa wadogo . Wengi wa wasichana tunaokutana nao hawana hata viatu vya kuvaa shuleni, kwa hivyo nina uhakika kabisa kwamba Yesu atachukulia kile unachokifanya kwa ajili yao kana kwamba kilifanywa kwa Yesu mwenyewe.

 

"Mfalme atajibu, ' Amin nawaambieni  kadri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu, mlimtendea mimi." Matthew25:40

 

Ni suluhisho la kushinda pande zote  ambalo litagharimu $45,000 kutekeleza! (Wazo lingine la mambo!) Chagua tu idadi ya wasichana unaotaka kubadilisha na kuzidisha kwa $15.

$30.00 kwa wasichana wawili $60.00 kwa wasichana wanne.                    $120.00 kwa wasichana wanane

Au shikwa na  "kichaa kidogo" na kusaidia shule nzima!

 

Unaweza pia kujitolea  kila mwezi kwenye mtandao wa www.farmstew.org ili kusaidia juhudi hizi na kazi yetu yote katika misingi inayoendelea!  

 

Ukichagua kutuamini kwa zawadi yako utakuwa ukiyarudia maneno ya Yesu wakati alipomuokoa mwanamke kutokana na aibu yake. Mchango wako utanena kwa hawa wasichana wa kiafrika,

 

"Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena. Marko 5:34

 

Mungu awabariki munapojihusisha na Utume Unaowezekana! 

Joy Kauffman, MPH

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa FARM STEW ya Kimataifa

 

P.S. Uchaguzi ni wenu wasichana  na maisha au bila maisha  ya siku zijazo.  Wale wanaohisi huwa hawana matumaini au wanaohisi kana kwamba wao ni mabinti wa Mfalme wa wafalme!

Edward, Mkurugenzi wetu wa nchi ya Uganda na gari iliyojaa visodo 2018 . Je, utatusaidia kujaza gari jingine na kusambaza?

 

* Majina ya wasichana yamebadilishwa kwa ajili ya faragha yao.


[1.] Taasisi ya Utafiti wa Sera za Chakula ya Kimataifa. 2016. Ripoti ya Ulimwengu ya lishe 2016: Kutoka ahadi hadi athari: kukomesha utapiamlo kifikia 2030. Washington, DC.

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Joy Kauffman, MPH
Joy ni mwanzilishi mwenye shauku wa FARM STEW.
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.

Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.