Kwa wakati kama huu ...
Timu za FARM STEW daima zimefundisha kunawa mikono na zilikuwa na vituo kama vile vilivyo hapa chini katika kila ofisi zetu. Tumeweka bomba la tippy katika maelfu ya nyumba. Ninajivunia sana timu zetu ambazo zinashiriki ujumbe wa maisha tele hata katikati ya wakati huu mgumu wa COVID-19.
Kwa kufuata maelekezo ya WHO kwa umakini wakufunzi wetu wanawajuza watu katika vijiji juu ya hatari na umuhimu wa vyote ambavyo tumewafunza hapo awali. Ukarimu na maombi yako hutuwezesha.

Wiki hii, wafanyakazi wetu walishiriki katika mafunzo ya Usafi wa Maji na wa Mazingira (WASH) kwa kushirikiana na Water4, Freedom Drillers, na FARM STEWI! Video hii ina maelezo kamili jinsi ya kunawa mikono vizuri! Tafadhali isambaze, hii inaweza kuokoa maisha. (Hii ilirekodiwa kabla ya taratibu za kutotangamana na watu.)
Kwa sababu ya rasilimali ndogo za huduma za afya na ukosefu wa mawasiliano, wakufunzi wetu wanawajulisha watu hatari ya COVID-19 na umuhimu wa yote tuliyowafundisha hapo awali. Tumewaandaa wakufunzi wetu kwa mwongozo (hapo chini) ambao tuliubadilisha kutoka kwa Kituo cha kuthibit magonjw (CDC) na Shirika La Afya Ulimwenguni (WHO) na kuongeza sehemu yetu wenyewe kuhusu kusaidia mwili wako kupambana na ugonjwa.
Wakufunzi wetu wanachapisha, kuunganisha na kuwaarifu (salama) jamii za vijijini ambao kwa kweli hawana taarifa kuhusu mambo yanayoendelea. Ukarimu na sala zako huwezesha. Asante!!

Ninawaalika msaidie kufanya kazi iwezekane kwa zawadi zenu za ukarimu hata katika nyakati hizi ngumu. www.farmstew.org/donate
Hatimaye, tunaendelea kuomba pamoja kwa ajili yako na kwa wale tunaowatumikia. Na tuwe mikono na miguu ya Yesu kwa walio katika mazingira magumu zaidi duniani, hapa nyumbani na katika sehemu ngumu za ulimwengu wetu.
Na amani ya Kristo itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu. (Wafilipi 4: 6-7),
Joy Kauffman, MPH
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji
FARMSTEW ya Kimataifa