Nijazie Maziwa ya Soya
"Akaita mtoto mmoja akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Bali, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi." Mathayo 18:2-5

Mtoto huyu ana shida ya utapiamlo wa nishati ya protini (Kwashirkor). Timu yetu ilikutana naye wakati ilipokuwa ikiendesha mafunzo katika kijiji chake wiki iliyopita, kijiji ambacho zaidi ya watoto 300 walifariki mwezi Januari 2015 kwa sababu ya utapiamlo baada ya kula kwa mda mrefu mlo wa unga wa muhogo na maji. Ugonjwa wa ukosefu wa protini ilikuwa ni neno litumikalo nchini Ghana ambalo linamaanisha "ugonjwa mtoto anao pata wakati mtoto mgeni anapozaliwa", ikimaanisha hivi ndivyo inavyotokea wanapoacha kunyonya maziwa ya mama yao kama chakula cha kimsingi.
Ndiyo sababu tumejitolea kustawisha vyakua vya kuachisha kunyonyesha vya mahindi, au muhogo, na soya, kwa ajili ya protini na kuanzisha matunda mengine na mboga kwa virutubishi vidogo.