FARM STEW yafaidika na tamasha la Adam Sabangan na ushuhuda wa familia
Tulibarikiwa sana na ujuzi na kujitolea kwa Adam Sabangan alipokuwa akielezea juu ya FARM STEW kupitia kwa wimbo!
Gratiela, mama yake Adamu alielezea mawazo yake katika Ushuhuda wa Familia ya Sabangan:
FARM STEW iko karibu na mioyo yetu! Hapa ziko sababu tano kwa nini sisi tulichagua kuunga mkono na kujihushisha na ujumbe wa FARM STEW.
- Utume wao ni wa kina. Kila kiungo katika kichocheo cha maisha tele kinahusiana na kinasaidia wengine. Wakati mawazo na fursa mpya zinapotokea wanatafuta kukubaliana na yale tu ambayo yanaingiliana na malengo yao.
- Wana Msisitizo mkubwa juu ya elimu. Kama mwalimu na mwanasaikolojia kielimu, hilo lilikuwa jambo ya kipekee kwangu. FARM STEW inaamini katika kuwapa watu ujuzi na maarifa ya kiutendaji. Kwa kukulia katika familia za wahamiaji, mimi na mume wangu tulihamasishwa umuhimu wa elimu na bidii sote tunashukuru kwa suala hili la FAMR STEW.
- FARM STEW ina umakini kuweka misingi yake ya elimu juu ya sayansi inayo aminika na kanuni za kibiblia.Pia wana mtazamo wa kutoa misaada na kueneza injili.
- Mungu anafungua fursa ili kuingia maeneo mapya. Mwaka huu wanapanga uzinduzi nchini Rwanda na Cuba. Hatutaki FARM STEW kupoteza fursa hii ya kushiriki kichocheo cha maisha tele
- Ni watu. Hebu tulikabili swala hili, shirika linaweza kuonekana la kiajabu kwenye karatasi au kwenye tovuti lakini si watu wanaoendesha ndio waletao tofauti? Tumegundua wafanyakazi wa FARM STEW ni baadhi ya watu wenye mvuto na wanyenyekevu ambao hutujawahi kuona wengine kama hao.
Asante kwa familia ya Sabangan!!