Mikono safi - Okoa Maisha - Hapa ni jinsi ya kufanya hivyo!
CoviD-19 inafagia ulimwengu. Najua haitatatua janga hili lakini, je, unajua kwamba kunawa mikono ni "njia rahisi iliyo na gharama nafuu zaidi kwa udhibiti wa magonjwa duniani kote"?
Miaka minne na nusu iliyopita FARM STEW imekuwa ikifundisha zaidi ya wahusika elfu themanini na moja jinsi ya kuosha mkono, jinsi ya kukohoa vyema, na usafi wa msingi katika kozi zetu za kiutendaji barani Afrika. Kwa msaada kutoka kwa watu kama wewe, idadi hiyo inaongezeka kila siku!
Sasa ni wakati wa FARMSTEW kuwa baraka kwako na familia yako!
Kutokana na virusi vya sasa vya COVID-19, ninakualika uchukue dakika chache unitazame nikifundisha somo la Usafi wa Mazingira la Mtandao la usafi la FARMSTEW, "Mikono Safi, Mwili Safi, Nyumba safi!" Ni mkusanyiko wa vyanzo vingi, ikiwa ni pamoja na shahada yangu ya uzamifu ya elimu ya kimataifa ya afya ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins (97').
Ninatoa maelekezo kamili na ya wazi kuhusu kunawa mikono, kukohoa kwa njia ifaayo katika kiwiko chako na kusafisha nyumba yako ili kuzuia magonjwa. (Baadhi inalenga nyumba za kiafrika lakini mengi kati yake ni muhimu kwako pia.)
Video hii iko katika kozi ya msingi ya FARM STEW (https://farmstew.teachable.com/) na jana niliiposti kwenye YouTube hapo chini ili kuieneza zaidi kwa upana!
Kwa muhtasari, kuna nyakati fulani ambapo ni muhimu sana kunawa mikono yako. WAKATI HUO NI SASA!!
Mtu yeyote akiwa mgonjwa nyumbani mwako au katika jamii, ni muhimu sana kunawa hata mara nyingi.
Bila ukarimu wa zawadi zenu kutoka kwa watu kama wewe, hatungeweza kamwe kuendeleza kozi hizi za kimtandao na kuzieneza bure. Zawadi yako leo inaweza kuokoa maisha!
Tafadhali fikiria kueneza makala haya kwani ujumbe huu ni muhimu kwa kila mtu na ni njia kubwa ya kujifunza na kuwaambia wengine kuhusu ujumbe wa FARM STEW.
"Kumbatio kubwa (halisi) kwa nyinyi nyote na muwe na amani ipitayo fahamu zote itokayo kwa Kristo pekee!