Iite utakavyo, bado ni Sudza
Hii ilikuwa ni ukweli wa kushangaza kupata kutembelea jamii za vibanda zinazoishi moja kwa moja pembeni mwa barabara kutoka kwenye hoteli ambapo tulikuwa tukikaa nchini Zimbabwe. Walikuwa wamechangamka zaidi; kwa sehemu fulani kwa sababu Steven na Dkt. Gil walikuwa tayari wamezuru mara chache.

Leo, tulipata kuwa huko wakati mama huyu mchanga aliye mjamzito alikuwa akitayarisha kifungua kinywa cha familia akitumia chembe za wanga za nafaka (SUDZA) na sukari kidogo na siagi ya njugu karanga. Shangwe mara tatu kwa ajili ya siagi ya njugu karanga, lakini nadhani wapendwa huenda watagawiwa robo kijiko ... protini yake haitoshelezi mtu yeyote na kwa kiasi kidigo kwa mwanamke mja mzito.