Ilichapishwa
Desemba 3, 2016

Aliyepitishwa na Mungu:Tofauti iliyoje Emmanuel anayoweza kufanya katika maisha!

Joy Kauffman, MPH

Kuchukuliwa na Mungu

Ina maana gani kweli ya kuchukuliwa na Mungu ... kuwa watoto wake na kuwa na uwezo wa kumlilia yeye kama Abba Baba? Picha ya rafiki yake Phionah, mkufunzi wa  FARM STEW ya Uganda pamoja na Shangazi yake inakuja akilini sasa ninapofikiria kuhusu kukubaliwa.  Alikuwa yatima kama msichana mdogo na kupelekwa kutoka nyumba moja hadi nyingine kwa ndugu zake wakubwa mpaka siku ambayo Shangazi yake alimchukua na ndugu yake Roger ili kuwalea.  Nilikuwa na fursa ya kuwa katika nyumba yao wiki iliyopita, nikalishwa kama malkia na kuwa na mtazamo wa upendo wa kweli kama ambavyo nimekuwa nikishuhudia mara moja moja katika maisha yangu. 

Phionah Bogere na Joy Kauffman

Phionah alikaa pamoja na Shangazi yake akituelezea kama wageni jinsi "yeye alivyo kila kitu kwakwe, mama yangu, Baba yangu, rafiki yangu."  Phionah alieleza jinsi Shanagzi yake alikuwa hajakula na bado waliweza kuhudhuria shule.  Jinsi mwanamke mmoja katika utamaduni ambaye hana nafasi kubwa kwa ajili ya ajira ya wanawake, alijitolea  kuleta chakula.  Yeye na Roger wamejitole maisha yao kuhakikisha kwamba wanamjali Shanagzi kwa upendo mwingi aliouonyesha kwa walipokuwa watoto.

 

Phionah, Shangazi na Roger katika nyumba ya kijijini

Phionah na Shangazi wakielezeana visa vyao 

 

Kisha siku ya pili, mimi nakutana na mvulana huyu mdogo mwenye kusikitisha  na nikaona maisha yaliyo na mkondo tofauti  mbeleni.   Tulikuwa tunatembea kwenye makazi ya mabanda ya Jinja kufanya baadhi ya ziara za nyumbani na tukamkuta na kaka yake karibu barabara ya reli chini tonobari ya plastiki, akilia.Tulimuuliza  mwanamke aliyekuwa akifanya kazi katika shamba lililokuwa karibu na ukagundua  kwamba mama yake na baba yake walikuwa wametalakiana na mamake kuondoka.  Kwa hivyo baba yake alikuwa akiwaacha siku nzima ili kwenda kutafuta kazi. Kipande kidogo cha muwa mkononi mwake ndicho riziki yake. Kijana huyu maskini na mwenye mateso alinivunja moyo wangu.  

 

Timu yetu ilirudi katika jamii hii jana ili kuwaongoza akina mama wa eneo hilo katika madarasa ya afya na lishe na kuwafundisha ujuzi wa kufanya maziwa  ya soya.  Tumaini langu na imani yangu halisi ni kwamba wanaweza kutumia ujuzi huo kwa  kulisha watoto wao na pia kuuza ili kupata baadhi ya mapato.   Ninaomba mtu awe na huruma kwa kijana huyu mdogo.  Sikuweza kumchukua pamoja nami nyumbani.

 

Yesu anajitolea mwenyewe.

Nilipokuwa nikisoma kitabu  kizuri cha maombi  jana usiku, sasa ikiwa ni maili 4,000 mbali na  roho hizi njema za wapendwa, nilifikiria juu ya Yesu na jinsi maisha yake ya upendo wa kujitolea binafsi ulifanya iwezekane kwetu sote kuchukuliwa kama watoto wa baba yake.   Ukweli kwamba hatatuacha au kutukataa kamwe ilinifanya nifikiri mvulana yule aliyeachwa. Tungekuwaje bila yeye.  

 

Katika sura ya kwanza ya Tumaini la vizazi vyote, tumepewa mtazamo wa upendo huu.  Ingawa Yesu alikuwa  amefurahia  milele ibada ya makundi ya malaika kila siku akiwa katika kiti cha enzi  mbinguni na baba yake tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu  alikubali kuwa maskini, mkimbizi,wa  kuwindwa, mtoto mwenye njaa akikimbilia  maisha yake huku wazazi wake wakimpeleka Afrika.  

 

"Katika kuchuchumia kwake kuchukua hali ya ubinadamu, Kristo alifunua tabia kinyume na tabia ya Shetani. Lakini bado alikuwa chini katika njia ya udhalilishaji. ' Tena alipoonekana ana umbo kama la mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti , naam,mauti ya msalaba ' Phil 2:8 "Ellen White anaendelea," kwa maisha yake na kifo chake, Kristo imefanikiwa hata zaidi ya kupona kutokana na uharibifu uliofanywa kupitia dhambi. Ilikuwa ni lengo la Shetani kuleta utengano wa milele kati ya Mungu na mwanadamu; lakini katika Kristo tumekuwa karibu zaidi tukiwa na umoja na Mungu kuliko kama hatungeanguka kamwe. Katika kuchukua asili yetu, Mwokozi alijifunga kwa binadamu na tai ambayo kamwe haiharibiki. Kupitia  umilele ameunganika nasi . . . Mungu ameweka asili ya mwanadamu katika utu wa Mwanawe na ameendeleza vivyo hivyo  katika mbingu ya juu. Ni "Mwana wa Adamu" ambaye alishiriki kiti cha  ufalme wa ulimwengu . . .  Katika Kristo familia ya duniani na familia ya mbinguni zimefungwa pamoja. Kristo aliyetukuzwa  ni kaka yetu, mbingu inajumuishwa katika ubinadamu na ubinadamu umefunuliwa katika kuwa karibu sana na upendo usio na mwisho. "

 

Ninashukuru sana kwa ajili ya kupitishwa kwangu katika familia ya Mungu kwa ajili ya nafasi yangu katika kuwa karibu sana na upendo usio na mwisho. Najiunga  na Phionah na upendo wake mzuri  akisema, "Yesu ni kila kitu kwangu, mama yangu, baba yangu, rafiki yangu."   

 

Nilijifunza wiki iliyopita kwamba Phionah  ambaye alikuwa akihisi upendo mwingi sana kutoka kwa halati yake ana eneza upendo huu kwa kuwatuma wavulana wawili yatima  kwenda shuleni na ujira wake wa FARM STEW.   Amejitolea sana kiasi kwamba hakuwa hata na Biblia yake aliyoitaka yeye mwenyewe hivyo amebaki na yangu. :)

 

 Naweza zungumzia zaidi na zaidi  kuhusu Emmanuel ... lakini unaweza kusoma sura au hata kitabu chote hapa. Kumsifu Mungu Baba yetu ambaye ndiye mtoaji wa kila kipawa kizuri kwa watoto wake. Tuweze kushiriki kwa ukarimu baraka ambazo tunapata katika kifua cha upendo wake usio na mwisho.

Shiriki
Shiriki
Iliyotumwa na 
Joy Kauffman, MPH
Joy ni mwanzilishi mwenye shauku wa FARM STEW.
Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.

Kisa cha Naki
Uganda, Afrika
Manukuu
"Nina umri wa miaka kumi na minne (14) na nilianza hedhi mwaka huu. Siku yangu ya kwanza nilihisi aibu na nikakosa kwenda shule ... Si rahisi kupata visodo katika kijiji changu na vichache vilivyoko ni bei ghali. Visodo hivi vipya vitaweza kunisaidia nikiwa katika hedhi. Kwasababu vinaweza kutumika tena, sitakuwa na wasiwasi tena nitakapopata hedhi!"
Visodo

Uhuru kutokana na aibu

Kila siku maelfu ya wasichana wa Kiafrika huacha shule. KWA NINI?  Kwa sababu ya hedhi . Unaweza kuwasaidia wasichana hawa kuendelea na masomo yao  shuleni kwa  kuwapa visodo vinavyoosheka, chupi na kuwapa ujasiri kwa  dola kumi na tano ($15 ) kwa kila msichana  
Lengo letu ni   kuwafikia wasichana  5000 katika mwaka wa 2020!

Irene
Uganda, Afrika
Manukuu
Maisha ya Irene yatabadilishwa wakati zawadi zako zitakapoleta maji safi kwa jamii yake
Ishara ya maelezo
Kila dola  mbili ($2 )zinazopewa FARM STEW zitazidishwa kwa dola moja ($1) na Water4, hadi  dola elfu themanini na nne ($84,000).
Maji

Uhuru kutokana na Ugonjwa na kazi ngumu

Watu elfu 300 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Zawadi yako inaweza kutoa maji safi kwa dola kumi na tano ($15) kwa kila mtu.  Maji salama sio tu huimarisha afya; bali hutoa fursa kwa ajili ya FARM STEW, kwa ushirikiano na makanisa ya mtaa  kutosheleza kiu ya kiroho ya wale walio na mahitaji.