Mgogoro
Njaa, ugonjwa na umaskini husababisha mateso makubwa.
FARM STEW Uganda
Miradi yetu
Ili kufanikisha mabadiliko,tunaendelea kufanya kazi katika miradi ifuatayo.
Njaa
Utapiamlo unaendelea kuongoza kama mzigo wa kimataifa wa ugonjwa.
Umechangia karibu nusu ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano – zaidi ya Virusi Vya Ukimwi/ UKIMWI (VVU/UKIMWI), malaria na kifua kikuu pamoja.
Afrika Mashariki ni kanda katika ulimwengu unaoendelea yenye kiwango cha juu zaidi cha udomavu, kwa asilimia thelathini na tano nukta sita (35.6), hali ya mtapiamlo wenye athari kubwa isioweza kubadilishwa.
Kwa kujibu, FARM STEW ilianza na mkakati rahisi wa kuwalisha watoto.
Ugonjwa
Utapiamlo unawaweka watoto katika hatari kubwa ya kufariki kutokana na maambukizi ya magonjwa ya kawaida, huongeza mzunguko na ukali wa maambukizi hayo, na kuchelewesha kupona. Wanawake na watoto ni miongoni mwa idadi kubwa ya watu wenye hatari zaidi ya masuala haya ya utapiamlo. Mara nyingi husababisha vifo vya mapema. Watoto wa mashambani mara nyingi wana uwezo wa asilimia arubaini na tano(45%) zaidi ya uwezekano wa kifo.
Upungufu wa lishe huchangiwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na udongo usio na rutuba, usafi wa mazingira na kiwango cha chini cha lishe bora. FARM STEW hushughulikia mambo haya yote kwa kuzingatia siku1,000 za kwanza za maisha.
Sarah, mtoto mdogo hapo chini ana dalili za udumavu na ukosefu wa protini
Umaskini
Wakati idadi ya jumla ya maskini duniani imepungua katika miongo ya hivi karibuni, asilimia ya wale wanaoishi Kusini mwa Jangwa la Sahara imeongezeka kutoka 17.4% hadi 27.7%.
Umaskini uliokithiri, unaopimwa kwa dola 1.90 kwa kila mtu kwa siku, huathiri sana watoto.
Milioni 387, au asilimia 19.5 ya watoto duniani, wanaishi katika umaskini uliokithiri!
"Kwa kadiri ulivyofanya kwa uchache wa haya, umenitendea"
Yesu katika Mathayo 25:40
Ndiyo maana tupo na tunajali.