Kazi yetu katika

Uganda

Kwa nini?

Uganda

FARMSTEW haizingatii takwimu mbaya za Uganda na umaskini uliokithiri lakini juu ya uwezo uliopewa na Mungu nchini Uganda kustawi! Changamoto zinazowakabili familia za kilimo vijijini zinaweza kuonekana kuwa haziwezi kushindikana, tamaduni katika karne zote zimeangalia Biblia na asili yenyewe kama chanzo cha hekima. Huko tunapata kichocheo cha maisha tele na uendelevu. Kwa kusaga kutoka vyanzo hivi, FARM STEW inaweza kuwaandaa watu walio katika mazingira magumu na ujuzi unaohitajika ili kuboresha maisha yao na nchi yao kwa ujumla.

Changamoto

Waganda wana tarajio la kuishi la  miaka 59 tu. Kwa nini?

  • Uwezekano wa kufa kwa watoto wadogo ni asilimia  arubaini na tano (45%) kiwango kilicho  cha  juu katika maeneo ya mashambani
  • Matumizi ya protini na virutubishi vidogo haitoshi
  • Mifumo ya maji na usafi wa mazingira unakosekana
  • Ukosefu  wa lishe bora huigharimu Uganda dola milioni mia nane  na tisini na tisa ($899,000,000) kwa mwaka
  • Asilimia thelathini na nane (38%) ya watoto chini ya miaka 5 wanakabiliwa na ukosefu wa lishe bora (udumavu)

Tunachofanya

Kufunza vijiji vyote kuhusu lishe, kilimo na desturi zingine za afya

  • Kufundisha jinsi ya kupata lishe bora inayopatikana nchini
  • Kuwahamasisha wenyeji kufuata tabia za msingi za usafi wa mazingira
  • Kusambaza visodo kwa wasichana, kuepuka kuacha shule na aibu
  • Kuwezesha familia na vifaa na mbegu kwa mashamba madogo endelevu
  • Kutoa mafunzo kwenye vijiji vya mashambani, shule, makanisa, misikiti na magereza
Miradi yetu

Katika 

Uganda

Miradi ifuatayo inaeleza jinsi tunavyofunza viungo vyetu vinane kwa wenyeji. Jifunze zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kuhusika.

Mradi huu |
Inaendelea
Inaishia
Maji
Irene ni mmoja wapo wa watu  663,000,000 ambao hawana uwezo wa kupata maji safi. Pampu ya maji kijijini mwao ilivunjika miaka iliyopita, pamoja na asilimia  thelathini (30%) ya pampu zote barani Afrika. Sasa FARM STEW inatoa chanzo cha matumaini kwa hali ya maji ili kuzima kiu yao ya kimwili na kiroho ($15 kwa kila mtu).
Mradi huu |
Inaendelea
Inaishia
Septemba 18, 2025
Visodo vya kufulika kwa Wasichana
Ulimwenguni kote wanawake na wasichana wengi hawana uwezo wa kupata visodo i, vyoo safi binafsi, au njia safi za kujikimu wakati wa hedhi. Tunaleta  heshima kwa wasichana kwa kuwafundisha na kuwaandaa kwa kuwapa vifaa wanavyo hitaji.
Mradi huu |
Inaendelea
Inaishia
Mashamba madogo ya familia 
Ili kuwezesha familia za mashambani kuwa na kujitegemea na kutoa fursa kwa biashara, tunasambaza mbegu za kuanzia na vifaa vinavyohitajika kuanzisha ukulima wa mashamba madogo. Wanafanya mengine yaliyo salia kwa msaada wa wakufunzi wetu wa FARM STEW!
Mradi huu |
Inaendelea
Inaishia
Mafunzo
Wakufunzi wetu wa FARM STEW wanasisitiza kanuni za kila mojawapo ya viungo vyetu vinane katika madarasa tunayoyafunza. Shughuli za kiutendaji hufanya masomo  kuchangamsha na kuwasaidia washiriki kustawi!

Tunachofanya

Kufundisha Mazoea Bora ya Afya na Maadili ya Kibiblia

Tunatumia viungo vyetu vinane ili kusaidia kuathiri maisha ya familia za mashambani vijijini nchini Uganda, na mafunzo ya kiutendaji katika vijiji vyao

F
Kilimo
Uaminifu kwa kanuni zilizofunuliwa katika neno la Mungu na zinazozingatiwa katika asili
Zaidi →
A
Mtazamo
Uchaguzi wa kuishi njia ya Mungu, kuwa na nidhamu na kuwa na mtazamo chanya
Zaidi →
R
Pumziko
Kila usiku na kila juma kwa miili yetu na pia kuruhusu udongo kupumzika
Zaidi →
M
Chakula
Vyakula vinavyotokana na mimea, vyakula kamili visivyo kobolewa ambavyo familia inaweza kuvikuza wenyewe
Zaidi →
S
Usafi 
Katika miili yetu, kwa kuzingatia wanawake na chakula chetu na karibu na nyumba zetu
Zaidi →
T
Kiasi
Kiasi katika mambo mema, kujiepusha na mambo ambayo ni ya hatari
Zaidi →
E
Ujasiriamali
Kutoa fursa, kushughulikia jinsia, kufuatilia uendelevu
Zaidi →
W
Maji
Safi, kuondoa sumu mwilini na wingi wa nafaka, mikunde na kwa ajili ya miili yetu
Zaidi →
Uganda

Timu

Hawa ndio watu wanaoleta ujumbe wa FARM STEW kwenye eneo hili.

Betty Mwesigwa
 Mkufunzi wa FARM STEW
Dan Ibanda
Kaimu Mkurugenzi wa Shamba la STEW Uganda
Daniel Batambula
 Mkufunzi wa FARM STEW
Edward Kawesa
It na Afisa Ufuatiliaji na Katibu wa Bodi
Eunice Nabirye
Makarani wa Kuingiza takwimu
Gideoni Birimuye
 Mkufunzi wa FARM STEW
Joanitar Namata
 Mkufunzi wa FARM STEW
Jonah Woira
Kiongozi wa Kilimo wa FARM STEW Uganda 
Juliet Ajambo
 Mkufunzi wa FARM STEW
Dkt. Mark Waisa
Rais wa Bodi ya  FARM STEW Uganda
Phionah Bogere
Mkufunzi wa FAMR STEW, Usafi wa Mazingira 
Robert Lubega
Mtaalamu wa kilimo na Mkufunzi wa FARM STEW 
Steven Mugabi
 Mkufunzi wa FARM STEW
Betty ana shahada katika Upishi na Usimamizi wa hoteli kutoka  Chuo Kikuu nchini Uganda! Yeye ni kiongozi mwenye talanta, mfanyakazi wa bidii na mama wa watoto watatu.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Betty Mwesigwa
+
Betty Mwesigwa
 Mkufunzi wa FARM STEW
Dan ni mhitimu wa chuo kikuu cha Bugema katika masomo ya Maendeleo. Yeye ana shauku kwa Yesu na kwa maskini. Anaongoza timu ya Iganga. Anapenda kuwasaidia wengine na kufanya kazi na wengine.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Dan Ibanda
+
Dan Ibanda
Kaimu Mkurugenzi wa Shamba la STEW Uganda
Dan ni kijana mwenye akili kali na moyo unaolenga kufikia! Ana shauku kwa jamii ya viziwi na anataka kuwaona wanajifunza mapishi ya maisha tele. Pia ana jicho makini kwa biashara.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Daniel Batambula
+
Daniel Batambula
 Mkufunzi wa FARM STEW
Dk. Mark hufanya kazi  kama Mkurugenzi wa shule ya Kiadventista ya Light  katika Busei Uganda. Amekuwa akijitolea  kwa timu ya FARM STEW  ya Uganda tangu mwanzo na alikuwa wa kwanza kumjulisha Joy kuhusu changamoto zinazowakabili wasichana kutokana na ukosefu wa usafi wa hedhi! Yeye anampenda Mungu na anajitahidi kuwa bora  katika yote ayafanyayo!
X
Jifunze zaidi kuhusu
Mark Waisa
+
Mark Waisa
Rais wa Bodi ya  FARM STEW Uganda
Edward Kaweesa hajui siku yake ya kuzaliwa. Yeye na kaka yake mkubwa walilelewa na mama asiye na mume, fundi wa cherehani aliyekuwa amehamia nchi ya Kenya ingawa yeye ni Mganda. Alihudhuria shule ya msingi ya Kiadventista ya Karura. Mama yake alifariki alipokuwa na umri wa miaka kumi na mmoja (11) na baba yake, ambaye alimuona mara tatu tu katika maisha yake, alifariki alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwil (12).  Aliendeleza masomo yake katika shule ya upili  kwa kukosa kuhudhuria shule kwa siku mbili kila juma ili kwenda kujitafutia karo na kuhudhuria siku nyingine tatu. Baada ya kuhitimu, alianza kufanya kazi kama mhudumu wa biashara ya mtandao wakati  alipokuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Busoga. Alipata Shahada ya Uandamizi  katika teknolojia ya habari. Alijifunza masomo mengi juu ya uaminifu kwa Mungu wakati wa masomo yake na pia alijifunza kutodharau kazi yoyote ndogo kamwe. Mambo yote yanaweza kufanyika kwa utukufu wa Mungu. Edward anahudumu kama Rais wa FARM STEW Uganda.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Edward Kawesa
+
Edward Kawesa
It na Afisa Ufuatiliaji na Katibu wa Bodi
Mimi ni Nabirye Eunice, nina umri wa miaka 21. Hapo zamani nilifanya kazi na Hospitali ya New Hope kama mhudumu wa maabara ya matibabu nikifanya kazi na watu. Kushughulika na wagonjwa hunipa furaha, hasa wagonjwa ambao wanaonekana kutokuwa na msaada. Nilifurahia kuwaelezea neno la Mungu ambalo liliwapa matumaini wakati walipoondoka hospitalini. Nilipokuwa bado nikifanya kazi katika Hospitali ya New Hope, niliweza kuingiliana na kiongozi wa timu ya FARM STEW Iganga, Daniel Ibanda, ambaye alinielezea kichocheo cha FARM STEW na hii ilikuwa sehemu iliyonivutia. Alinisababisha kufanya kazi kwa hiari na FARM STEW, hasa nilipokuwa siko katika zamu kazini hospitali. Nilihudumu kwa furaha kwa kujitolea karibu mwaka mmoja. Ninafurahi kwamba sasa nimeajiriwa katika FARM STEW kama mfanyakazi wa kudumu. FARM STEW imenisaidia kubadilisha mtazamo wangu, kwamba ninaweza kufanya mambo yote katika Kristo anitiaye nguvu. Imenisaidia kutimiza ndoto zangu za kuitumikia jamii. Nimeboresheka katika ujuzi wa jinsi ya kuingiza tarakwimu na usimamizi wa nakala. Kama FARM STEW inavyoendelea, nitajaribu kufanya vizuri zaidi.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Eunice Nabirye
+
Eunice Nabirye
Makarani wa Kuingiza takwimu
Gideon Birimuye ni mkufunzi mwenye FARM  STEW Uganda; kampuni tanzu ya FARM STEW ya Kimataifa, ambayo dhamira yake ni kuboresha afya na ustawi wa familia  ndogo za vijijini ulimwenguni kote. Gideon ni mwanachama wa ASI kitengo cha Jinja na pia kwa upande mwengine  ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kanisa la SDA la kati laJinja na Maranatha Radio, shirika la vyombo vya habari linayojitahidi kuimarisha na kusukuma tume ya injili ili watu wote wa Mungu waje kuujua ukweli. Mbali na mahusiano yake makubwa ya umma na uzoefu wa masoko, Gideon ni mjasiriamali na kocha wa biashara. Gideon ni mtaalamu wa CCNA aliyethibitishwa kutoka Chuo Kikuu cha Makerere. Alihitimu na tuzo ya heshima  kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbarara akiwa na Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Kompyuta.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Gideoni Birimuye
+
Gideoni Birimuye
 Mkufunzi wa FARM STEW
Joanitar ni baraka kwa wale wote walio karibu naye. Alianza kazi yake na  FARM STEW kama mhudumu wa kujitolea na kwa haraka alijifanya sehemu muhimu ya timu.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Joanitar Namata
+
Joanitar Namata
 Mkufunzi wa FARM STEW
Jonah ni mtaalamu wa maua mwenye shauku kwa watu na miti. Anapenda kuwasaidia watu kupitia kilimo.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Jonah Woira
+
Jonah Woira
Kiongozi wa Kilimo wa FARM STEW Uganda 
Juliet ni wa furaha. Moyo wake ni mkubwa sana na huushirikisha kwa uhuru hasa na jamii yake ya viziwi.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Juliet Ajambo
+
Juliet Ajambo
 Mkufunzi wa FARM STEW
Mpendwa Phionah ni msichana wa ajabu ambaye amenawiri kama mkufunzi wa FARM STEW. Alikuwa yatima kamili katika umri mdogo sana. Unaweza kuona kisa chake cha kuvutia na shangazi yake mpendwa hapa: https://www.youtube.com/watch?v=yuYomKc3C-0 Kukutana na Phionah ni baraka na yeye huangaza upendo wa Yesu kwa wote ambao hukutana naye. Sasa anatumia mshahara wake wa FARM STEW kuwasaidia wavulana wawili yatima.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Phionah Bogere
+
Phionah Bogere
Mkufunzi wa FAMR STEW, Usafi wa Mazingira 
Robert Lubega ndiye aliyemfanya Joy kutambua kuwa FARM STEW  iliwezekana. Alikuwa wakala wa Ugani wa Kilimo kwa vyama vya ushirika vya wakulima wa eneo hilo nililopangiwa wakati nilipokuwa nikijitolea kwa mpango wa Mkulima kwa Mkulima wa USAID. Alikuwa akihudumu kama mfasiri wangu nilipokuwa nikiendesha madarasa ya lishe na kupika, akihusisha soya na mboga kwa kutumia Biblia kama maandishi yetu ya msingi. Lakini alikuwa zaidi!! Nilipoanza kusema kidogo  aliongoza zaidi ki darasa, matokeo ya jamii yalikuwa mazuri sana. Robert alijifunza haraka sana na hivi karibuni alikuwa akinifundisha ukweli husika kuhusu kilimo! Alifurahishwa hasa na ukweli kwamba, isipokuwa kwa taarifa ambayo ilikuwa ya vitendo na inayotumika mara moja , hatukuwa tukileta chochote kutoka nje ya kijiji. Uwezeshaji wake ulinifanya nitambue kwamba viongozi wa eneo hilo wanaweza kufanya madarasa katika lugha yao yao ya kienyeji na kwa kufanya hivyo kuteka  usikivu na mioyo ya washiriki wa darasa. Ninashukuru kwamba Robert na wanachama wote wanne wa awali wa timu ya FARM STEW Uganda bado wanaendelea na maono! Hapa hapa: https://www.youtube.com/watch?v=-e03Dbt7yTI&t=3s
X
Jifunze zaidi kuhusu
Robert Lubega
+
Robert Lubega
Mtaalamu wa kilimo na Mkufunzi wa FARM STEW 
Steven ni mkufunzi mahiri, mkulima na mjasiriamali. Yeye ni baba wa watoto wanne na kiongozi wa kwaya ya watoto.
X
Jifunze zaidi kuhusu
Steven Mugabi
+
Steven Mugabi
 Mkufunzi wa FARM STEW
KILIMO
MTAZAMO
PUMZIKO
MILO
USAFI
KIASI
UJASIRIAMALI
MAJI