Maadili yetu
FARM STEW inaongozwa na maadili matano ya msingi.
1
MTAZAMO WA FAMILIA MASHAMBANI
Ulimwenguni kote,, familia zilizo hatarini zaidi ziko vijijini na zinalima ili kujikimu. Walio katika hatari zaidi ya maisha haya wako katika siku1,000 zao za kwanza ambapo bado wako tumboni, mgongoni mwa mama yao na nyumbani au shambani. Hakuna programu au huduma itakayowafikia isipokuwa iwafikie wazazi wao kwanza. Kuwafikia ni kipaumbele chetu cha juu.
2
MPANGO
Tuna nia ya kujenga uwezo wa wakulima wadogo na jamii kuchukua hatua katika kushughulikia changamoto zao kwa pamoja zinazohusiana na shughuli za afya ya umma katika lishe, kilimo endelevu, maji, usafi na biashara.
3
Ubunifu
Tunalenga kutoa mikakati rahisi ya ndani ambayo husaidia jamii ndogo za kilimo kukuza suluhisho ambalo litaimarisha mbinu zao za kilimo, desturi za afya ya umma na changamoto shirikishi wanazokumbana nazo katika maisha na mifumo yao.
4
KUHESHIMU HEKIMA YA KALE
Katika kila kitu FARM STEW hukuza, kwanza tunatafuta njia ya kale. Tunawahimiza jamii kuuliza, Je, kuna hekima katika jinsi mababu zetu walivyofanya vitu hivi, Je, kuna hekima katika Biblia au hekima katika asili ambayo tunaweza kujifunza kwayo? Wakati wowote inapowezekana huunganisha uvumbuzi kwa njia za kale.
5
UADILIFU
Tunajiona kuwa, Kama Wakristo, tuna kiwango cha juu cha uadilifu wa kibinafsi na kishirika. Tunaunda nafasi ya kuheshimu maadili ya jamii, wakati tukihimiza mabadiliko yanayochangia maendeleo ya jamii na kumtambulisha Mwokozi mwenye upendo na Mungu Mtakatifu.
Tunao watumikia
Kila mmoja
Sisi ni Wakristo wanaofanyakazi kote ulimwenguni kutumikia kila mtu bila kujali imani zao.
miradi ya sasa
miradi inayoendelea