Historia
FARM STEW ilizinduliwa nchini Uganda katika msimu wa vuli mnamo mwaka2015. Joy Kauffman, MPH, mtaalamu wa Lishe na stashahada ya Afya ya Umma kutoka Chuo Kikuu Cha Johns Hopkins, na ya kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Illinois alipokuwa akihudumu na Mkulima wa USAID kwa mpango wa Mkulima nchini Uganda. Zoezi rasmi la Joy lilikuwa ni kufanya kazi na vyama vya ushirika vya kilimo ambavyo wanachama wake 60,000 walikuwa wameamua walitaka msaada wa kujifunza kusindika maharage ya soya wanayolima.
Mara tu alipokuwa Uganda, kwa kushirikiana na watu wanaojitolea, Joy alifunza madarasa ya lishe kiutendaji na madarasa ya kupika akiangazia soya na mboga kwa akitumia Biblia kama maandiko yetu ya msingi. Katika kipindi cha mafunzo ya siku mbili, tuliwafunza misingi ya vyakula vya mimea visivyokobolewa (ambavyo ni muhimu kama ilivyo washiriki wengi hula mboga kulingana na mahitaji ya kiuchumi), lishe ya mtoto, na umuhimu wa kuloweka nafaka na kunde ili kuongeza upatikanaji wa virutubishi vya madini. Pia tulikuwa na darasa la upishi kiutendaji: kutengeneza maziwa ya soya, kwa kutumia mabaki ya , "okara" kama unga wa kuongezwa kwenye uji (busera na posho), kula soya ya kijani (edamame), na mboga zenye rangi mbali mbali kama upinde na maharage ya kupikwa ya soya isiyosindikwa.
Mwitikio wa jamii ni wa kutia moyo sana.
Watu wa kujitolea wa Uganda walikuwa hasa wamechangamshwa na ukweli kwamba, isipokuwa kwa taarifa ambayo ilikuwa ya vitendo na iliyotumika mara moja, tulikuwa hatuleti chochote kutoka nje ya kijiji. Muda ulipoendelea ilikuwa ni vizuri kuona mwingiliano na uwezeshaji wenye ujuzi ambao ulitokea kwa kawaida wakati viongozi hawa walifundisha madarasa katika lugha yao ya kienyeji. Waliteka nyara umakini na mioyo ya washiriki wa darasa.
Hapo ndipo Joy alitambua kwamba mafunzo haya yanaweza kuokoa maisha ya watoto wengi mno bado alihitaji kurudi nyumbani kwa mabinti zake. Alishindana na ukweli kwamba katika Afrika watoto 5 chini ya umri wa miaka mitano hufa kila dakika! Alimwomba Mungu afanye nini na katika maombi, alihisi sauti tulivu, ndogo inasema, "waajiri."
Joy alionyesha kuwa tayari lakini alijenga uwezekano bila kumwambia yeyote kile alichoshawishika kukifanya
Pamoja na wenyeji, walianza kuzalisha vifaa vya maelekezo ya hali ya juu, ambayo tunaweza kutoa kama zawadi kwa jamii ambazo tulifundisha. Kwa njia hii, tangu mwanzo tungefunza wakufunzi na kuzidisha kazi. Edward Kaweesa, mmiliki wa duka la kompyuta nchini alikuja kuwaokoa. Alibadilisha mawazo ya Joy kuwa michoro ambayo ilizungumza wazi, kuwasilisha habari za afya na lishe, kwa njia inayofaa kitamaduni. (Edward sasa anahudumu kama Mkurugenzi mkuu wa FARMSTEW nchini Uganda.)
Wazo la timu lilianza kupata mwelekeo na kukamilika wakati Joy alipohubiri katika Kanisa Sabato yake ya mwisho na kukutana na Betty Mwesigwa, mwanamke mwenyeji ambaye alikuwa na maarifa makubwa ya kusindika soya aliyojifunza alipokuwa akisoma katika Chuo akijisomea shahada ya Lishe, Upishi na Usimamizi wa Hoteli katika Chuo Kikuu cha Bugema. Mchana huo huo mwanamke mchanga, Phionah Bogere, alimsogelea Joy wakati wa darasa la kujifunza kupika akisema, "Ninataka kuwa mmoja wa timu yako." Hii ilikuwa kabla ya Joy hajamwambia kwa mtu yeyote kwamba Roho Mtakatifu alikuwa tayari ameweka moyoni mwake kwamba lazima timu iundwe kuendeleza kazi.
Katika miezi kumi ya kwanza, Joy alifadhili FARM STEW kwa kutuma mshahara wake ulioajiri timu ya Uganda ya wakufunzi watano. Alikuwa msimamizi wa ruzuku ya USDA kwa idara yake ya afya ambayo ilimruhusu kufanya kazi na wakulima wadogo wadogo katika kukuza mazao katika masoko ya wakulima na chakula cha mboga kijijini Illinois. Malengo sawa yalifanya kuwa rahisi kuiunganisha kazi na FARM STEW .
Mwezi Machi 2016 FARM STEW ilichunguza uwezekano nchini Zimbabwe ambako ilikutana na Dkt. Arlene Vigilia ambaye alikuwa mwanachama mwanzilishi miezi michache baadaye wakati FARM STEW Kimataifa ilikua na kuwa shirika huru la misaada, lisilo la kifaida 501(c) 3,. Kwa bahati mbaya Dk. Vigilia alifariki Mei 2017 na tutamkosa milele. Shauku yake ya Yesu na njia yake ya kuwafikia watu kupitia huduma kwa mahitaji yao bado huwatia moyo wote wanaohusika leo.
Mwezi Machi mwaka wa 2017 tulizinduliwa timu ya pili ya wakufunzi wa Jinja, Uganda, chanzo cha mto Nile. Mwezi Machi ya 2018, FARM STEW ilizinduliwa Zimbabwe na katika kambi za wakimbizi kaskazini mwa Uganda. Hivi karibuni Desemba 2018, tulizindua timu huko Sudani Kusini kwenyewe.
FARM STEW Uganda, Zimbabwe, na Sudan Kusini zote ni taasisi zilizosajiliwa kisheria katika nchi zao. Tumebarikiwa na bodi iliyo na mchanganyiko mbalimbali na wafanyakazi wachache ambao wamejitolea sana kwenye kazi hiyo.
Utukufu kwa Mungu tunapotafuta hekima na utambuzi kutoka kwake kwa ajili ya siku za baadaye za FARM STEW